BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MBUNGE WA CCM AFARIKI DUNIA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI DAR ES SALAAM.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh19cKg-6VyVcj9WcFGCMfEYi3C1k5xuPxrCND4JCaHX_iko6k8TYrs11ov1MjDWsbrwfOX9ypqAttfG76DrgwsTdItQHB-QbaXX_did0mZAXihZ7xaNJ4KCgYKQkLO6W7-GPxsxlHMY3s-/s1600/1.png 

Rais Jakaya Kikwete kushoto akimjulia hali aliyekuwa mbunge wa Geita Marehemu Donald Max enzi za uhai wake.

Dodoma.
Mbunge wa Geita (CCM), Donald Max (58) amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.



Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema kuwa mbunge huyo (pichani) alifariki jana saa 12.00 jioni katika hospitali hiyo.

Ndugai alisema Max alikuwa mahututi kwa kipindi cha takribani miaka miwili iliyopita.


“Taratibu za maandalizi ya mazishi kwa sasa bado maana ni kama dakika 15 zilizopita ndiyo kafariki,” alisema Ndugai.


Max alizaliwa Mei 22 mwaka 1957 na kusoma katika Shule ya Msingi ya Salvatorian Convent na baadaye kujiunga na Shule ya Sekondari ya Azania mwaka 1971 hadi mwaka 1974.


Mwaka 1980 alikwenda nchini Urusi na kusoma kozi ya ufundi katika Chuo cha Ufundi cha Roston on Don kabla ya kujiunga na Taasisi ya Volgograd Polytechnical nchini humo na kutunukiwa Shahada ya Uzamili katika Uhandisi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: