OCD wa Arusha
Gilles Mulloto kushoto akizungumza jambo mbele ya Mbunge wa Arusha Godbless Lema katika picha ya maktaba.
Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas, amesema tuhuma alizotoa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) kuwa jeshi lake linamwonea kwa kumkamata na kumuweka mahabusu ovyo, wakati yeye sio mhalifu siyo za kweli na kwamba Mbunge huyo amekuwa chanzo cha vurugu katika uandikishwaji wa daftari la wapigakura.
Sabas alisema jana kuwa Lema anasababisha vurugu kwa kutembelea maeneo ambayo watu wamejitokeza na kujiandikisha na kuhutubia, kitu ambacho ni kinyume cha sheria.
“Yeye kama anataka kuhamasisha watu hatukatai, aende maeneo ambayo daftari bado halijafika akahamasishe na likifika aache wananchi wajiandikishe na siyo kuwafuata kwenye mistari na kuanza kupiga hatuba, siyo sahihi,” alisema.
Aliongeza: “Kwanini anapokuwapo Lema vurugu zinatokea, asipokuwapo hakuna vurugu, yeye asiende kwa watu ambao tayari wamejitokeza kujiandikisha, aende kwa ambao bado hawajafikiwa na daftari hilo.”
Sabas alisema kuwa Jeshi la polisi haliwezi kuonea mtu wala yeye (Lema) isipokuwa likipata taarifa kama siku ya tukio ya Juni 20 alipokamatwa kuwa analeta vurugu na wananchi hawataki kumwona katika maeneo ya uandikishaji ndipo walipokwenda kumkamata.
Alisema siku ya tukio walipata taarifa kutoka kwa askari walioko doria kwenye kituo cha Olsunyai kuwa kuna vurugu zinazofanywa ma Mbunge huyo na kuomba ulinzi uongezwe na askari wakapelekwa zaidi na kumtia mbaroni na wenzake 24 na aliyetoa taarifa polisi aliomba ulinzi.
“Lakini pia Lema anaongozana na kundi la watu toka maeneo tofauti ya uandikishaji, kitu ambacho siyo sahihi pia nacho kinakera baadhi ya watu,” alisema.
Hata hivyo, alisema uchunguzi dhidi ya tuhuma zake unaendelea na ukikamilika atachukuliwa hatua stahiki. CHANZO: NIPASHE
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kitaifa
/ MBUNGE WA CHADEMA JIMBO LA ARUSHA MJINI GODBLESS LEMA NDIYE CHANZO CHA VURUGU KATIKA UANDIKISHWAJI DAFTARI LA WAPIGAKURA.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment