BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MISIKITI 80 YA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMA KUFUNGWA NDANI YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI NCHINI TUNISIA.

null 
Utawala nchini Tunisia unasema kuwa utafunga misikiti 80 katika kipindi cha wiki moja inayokuja kwa madai ya kuhubiri chuki na jihad.


Hii ni kufuatia shambulizi lililofanyika kwenye hoteli moja hapo jana ambapo takriban watu 39 wengi wao wakiwa raia wa mataifa ya ulaya waliuawa na mwanamme mmoja aliyejifanya kuwa mtalii.

Wapiganaji wanaoshirikiana na wanamgambo wa Kundi la kiislamu la Islamic State wamesema kuwa wao ndio waliotekeleza shambulizi hilo. Miili ya watalii ilikuwa imetapakaa ufukweni

nullMpiganaji mmoja alijifanya kuwa mtalii kabla ya kuwafyatulia risasi watalii ufukweni 

Waziri mkuu nchini Tunisia Hanib Essid anasema kuwa misikiti hiyo ndio iliokuwa ikitumika kueneza propaganda na kuunga mkono ugaidi. Waziri mkuu ametangaza kuwa misikiti hiyo ndiyo imekuwa ikihubiri Jihad
Hali ya usalama umeimarishwa maradufu katika maeneo mengi mjini Tunis na karibu na majengo yenye watalii wengi.
Mpiganaji mmoja alijifanya kuwa mtalii kabla ya kuwafyatulia risasi watalii ufukweni

Tayari wanajeshi wa akiba wameamrishwa kuripoti mara moja katika kambi za jeshi zilizoko karibu nao.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: