BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NDEGE YA KIJESHI YAANGUKA NA KUUA ABIRIA 100

Takriban watu 100 wameuawa baada ya ndege ya uchukuzi wa kijeshi ya Indonesia kuanguka mapema leo katika maeneo yenye makazi ya watu huko Medan Sumatra.



Maafisa wa kijeshi wanasema kuwa tayari miili 49 imepaa na katika eneo la ajali.

Maafisa wa kijeshi nchini Indonesia, wanasema kwamba ndege hiyo ya uchukuzi ya majeshi ya taifa hilo, ilianguka muda mfupi baada ya kupaa angani.


Ndege hiyo ya kubeba mizigo aina ya Hercules 130 ilikuwa na wahudumu 12 na abiria 113 ilipoanguka.

Afisa mkuu wa jeshi la wanahewa Air Marshall Agus Supriatna amesema kuwa hakuna manusura waliopatikana hai.

Kuna ripoti kuwa watu bado wanasikika wakipiga mayowe katika majengo yaliyoanguka.

Ndege hiyo iliharibu kabisa nyumba ambazo iliziangukia katika mji wa Medan, kaskazini mwa jimbo la Sumatra.

Picha za runinga na kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha moto unatoka kwenye mabaki ya ndege hiyo.

Msemaji wa jeshi la angani alisema kuwa rubani alikuwa ameomba kurejea katika uwanja wa kambi ya kijeshi kwa sababu ya matatizo ya kimitambo.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: