BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ZIARA YA KINANA KANDA YA ZIWA YAPOKELEWA NA SUNGUSUNGU KWIMBA MKOANI MWANZA.

Komredi Kinana akiwaongoza Sungusungu mara baada ya kulakiwa na wananchi katika Kijiji cha Hungumalwa.
Komredi Kinana akivishwa kofia ya jadi ya Sungusungu wakati wa mapokezi wilayani Kwimba.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akilakiwa na Kikundi cha Ulinzi wa Jadi cha Sungusungu, alipowasili katika Kijiji cha Hungumalwa njaia panda ya Mwamashinga alipoanza ziara Jimbo la Kwimba, mkoani Mwanza, ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG Komredi Kinana akipuliza filimbi mara baada ya kuvishwa mavazi ya asili wakati wa mapokezi wilayani Kwimba jana.
Mbunge wa Jimbo la Kwimba, Shanif Mansoor akielezea mbele ya Komredi Kinana jinsi alivyosaidia kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo hilo.
Komredi Kinana akiangalia ngoma iliyokuwa ikitumbuiza wakati wa kukaguaujenzi wa mradi wa Zahanati katika Kijiji cha Hungumalwa, katika Jimbo la Kwimba, mkoani Mwanza.
Mbunge wa Jimbo la Kwimba, Shanif Mansoor akishiriki ujenzi wa Zahanati ya Hungumalwa iliyokaguliwa na Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Kinana
Wananchi mjini Ngudu, Kwimba wakimlaki Komredi Kinana huku wakiwa na bando na kumsifu mbunge wao Shanif Mansoor.
Wananchi wakimlaki Komredi Kinana alipofika kushiriki uoandani wa miche ya miti ya Kikundi cha wajasiriamali mjini Ngudu, Kwimba
Komredi Kinana akishiriki kupanda miche ya miti katika kikundi hicho kilichopo mjini Ngudu, wilayani Kwimba.
 


Komredi Kinana akifungulia maji alipofika kukagua ukamilishwaji wa ujenziwa mradi huo eneo la Majengo Mapya, mjini Ngudu, wilayani Kwimba
Mmoja wa akina mama wa Majengo Mapya mjini Ngudu, katika Jimbo la Kwimba akitwishwa ndoo ya maji na Komredi Kinana baada ya kuufungua mradi huo.
Mbunge wa Jimbo la Kwimba, Shanif Mansoor akisaidfia kumtwisha ndoo ya maji baada ya Komredi Kinana kuufungua mradi wa maji eneo la Majengo Mapya, mjini Ngudu wilayani Kwimba.
Wauguzi n madaktari wa Hospitali ya Wilaya ya Ngudu wakisalimiana na Komredi Kinana aliyekwenda kukagua jengo la wagonjwa mahututi (ICU), wakati wa ziara yake Jimbo la Kwimba, mkoani Mwanza jana
Komredi Kinana akisalimiana na Balozi Specioza Balele wa CCM Shina namba 12, alipomtembelea wakati wa ziara yake Jimbo la Kwimba katika Mji wa Ngudu.
Kikundi cha Ulinzi wa Jadi cha Sungusungu kikitumbuiza kwa ngoma ya asili wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM kwenye Uwanja wa Mpira wa Ngudu, wilayani Kwimba.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: