Chile imewashinda Argentina kupitia kwa mikwaju ya penalti na kushinda kombe kubwa zaidi kati ya nchi za Marekani ya kusini la Copa Amerika.
Chile ambayo ni waandalizi waliwashinda Argentina mabao 4-1 kupitia mikwaju ya penalti baada ya timu zote kukosa kufunga.
Ni miaka 22 tangu Argentina washinde kombe lolote kubwa kwenye mashindano ya kandanda ya kimataifa.
Mashabiki Mchezaji wa Arsenal Alexis Sanchez alifunga bao la ushindi baada ya mshambuliaji wa Argentina Gonzalo Higuain kupiga nje huku mkwaju wa Ever Banega ukinyakwa na kipa Claudio Bravo.
Awali Higuain alikuwa amekosa bao la wazi aliposalia na kipa baada ya dakika 90 za mchezo.
Messi kwa mara nyingine ashindwa kuipatia taifa lake taji Sanchez karibia afunge katika dakika za ziada.
Higuain akikosa penalti Miongoni mwa maelfu ya mashabiki waliojaa kuishabikia timu yao ni wachimba mgodi 33 waliokwama chini ya mgodi kwa wiki kadhaa mwaka 2010,katika kisa kilichovutia hisia nyingi duniani.
Wenyeji wa Copa America, Chile wametwaa ubingwa wa michuano hiyo baada ya kuwafunga Argentina kwa hatua ya mikwaju ya penalti katika mchezo mgumu wa fainali.
Timu hizo mbili zilitoka suluhu katika dakika 90 za kawaida na hata baada ya dakika 30 za nyongeza bado matokeo yalisomeka 0-0.
Hakukuwa na njia nyingine ya kumpata mshindi zaidi ya kupisha hatua matuta ambapo Chile wakaibuka wababe kwa penalti 4 kwa 1.
Lionel Messi alijikuta akikatwa sana kiatu katika muda mwingi wa mchezo kutoka kwa mabeki wa Chile huku Angel Di Maria akitolewa dakika ya 29 baada ya kuumia.
Gonzalo Higuain alikuwa miongoni wa waliokosa penalti. Wafungaji wa penalti za Chile walikuwa ni Matias Fernandez, Arturo Vidal, Charles Aranguiz na Alexis Sanchez wakati penalti pekee ya Argentina iliyotinga wavuni ni ile ilipigwa na Lionel Messi.
Mshambuliaji hatari wa Argentina Gonzalo Higuain alikuwa miongoni wa waliokosa penalti.

0 comments:
Post a Comment