BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAJESHI YA MAREKANI YAWATIA HASARA WANAMGOMBO WA KUNDI LA KIGAIDI LA AL SHABAAB NCHINI SOMALIA.

 

Viongozi wanne wa ngazi za juu wa kikundi cha wanamgambo wa Al Shabaab wameuawa leo Nchini Somalia kwa shambulio la bomu la angani.

Mmoja wa aliouawa alihusika na Shambulio la Tarehe 2 Aprili, 2015 katika Chuo Kikuu cha Garissa na kusababisha vifo vya wanafunzi 147




Watu katika mji wa Baardhere ulioko kusini mwa nchi hiyo wanasema walisikia milipuko asubuhi ya leo katika eneo hilo.

Kisha wapiganaji hao wa Al shabaab wakafika eneo hilo la tukio.

Baardheere ni moja ya miji ambayo bado ingali inadhibitiwa na wapiganaji wa Al shabaab.

Wanajeshi wa muungano wa Afrika na wale wa serikali ya Somalia wanakaribia eneo hilo.

Viongozi kadhaa wa kundi hilo wameuawa kwenye mashambulio ya mabomu ya angani yaliyoangushwa na wanajeshi wa Marekani.


Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: