BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

VIFUNGU VYA SHERIA VILIVYOFANYA KAZI YA KUWATIA HATIANI MAWAZIRI WA ZAMANI ENZI ZA RAIS MKPA, DANIE YONA NA BASIL MRAMBA KWENDA JELA MIAKA MITATU KWA KUITIA HASARA SERIKALI SH11.5 BILIONI.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgdLyy_0KupgkUfspWM7RFXLRH9uS0KQf2tN2mOznjxFCev71kx9sZHotd_qjRM0d4W0fzUEQRoUESD1Qs2sKC9FnhAfdNeLhBy8RFjZIavhixJcRQRSZecH3UNTm6Ppc6J8wPfmNdGSw5L/s640/Mramba+na+Yona.jpg

Mawaziri wa awamu ya tatu, Basili Mramba (aliyeketi) na Daniel Yona akipanda kwenye gari baada ya mahakama ya Kisutu kuwahukumu miaka mitatu jela na kulipa faini ya sh5 milioni.

Dar es Salaam. Mawaziri wawili wa zamani, Basil Mramba (Fedha) na Daniel Yona (Nishati na Madini), wamehukumiwa kila mmoja kifungo cha miaka mitatu jela na kulipa faini ya Sh5 milioni baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Sh11.5 bilioni.

Akisoma hukumu hiyo kuanzia saa 7.15 mchana hadi saa 8.11 mchana, Hakimu Mkazi, Sam Rumanyika alisema baada ya jopo la mahakimu watatu kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi 13 wa upande wa mashtaka na wengine sita wa utetezi wakiwamo washtakiwa wenyewe, wameamua kumwachia huru mshtakiwa wa tatu, aliyekuwa Katibu Mkuu wa zamani wa Fedha, Gray Mgonja.


 Hakimu Rumanyika alisema wanamuachia huru Mgonja kwa sababu upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka yote 11 yaliyokuwa yakimkabili.


Hakimu Rumanyika alisema wanamtia hatiani Mramba katika mashtaka yote 11 yaliyokuwa yakimkabili.


Alisema katika shtaka la kwanza hadi la 10 ambayo ni ya matumizi mabaya ya madaraka, atakwenda jela kifungo cha miaka mitatu jela kwa kila shtaka na vifungo hivyo vitakwenda sambamba, hivyo atatumikia kifungo cha miaka mitatu jela.


Katika shtaka la 11 ambalo ni la kuisababishia Serikali hasara ya Sh11.7 bilioni pia alitiwa hatiani na kuhukumiwa ama kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa fidia ya Sh5 milioni na kuwa vifungo hivyo vyote vitakwenda sambamba hivyo Mramba atatumikia kifungo cha miaka mitatu jela. Wakili wake Peter Swai alisema atakata rufaa.


Kuhusu Yona, Hakimu Rumanyika, alisema naye wanamtia hatiani katika shtaka la kwanza, la pili, la tatu na la tano ambayo ni ya matumizi mabaya ya madaraka pamoja na la 11 la kuisababishia hasara Serikali ya Sh11.7 bilioni.


 
Waziri wa zamani wa Nishati na Madini , Daniel Yona na Waziri wa zamani wa Fedha, Basil Mramba.

“Yona katika kila kosa atatumikia kifungo cha miaka mitatu jela na adhabu zote zinakwenda sambamba hivyo atatumikia kifungo cha miaka mitatu jela.


“Katika shtaka la kusababisha hasara atalipa fidia ya Sh5 milioni na iwapo atashindwa atakwenda jela miaka mitatu,” alisema Hakimu Rumanyika.


Ilivyokuwa
Kabla ya hukumu kutolewa, mawakili wanaowatetea washtakiwa hao, Swai anayemtetea Mramba na Eliasa Msuya anayemtetea Yona waliiomba Mahakama iwape adhabu nyepesi washtakiwa hao kwa sababu hilo ni kosa lao la kwanza, umri wao ni mkubwa Yona (76) na Mramba (75), wanaumwa na walikuwa wakitibiwa India wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo.


Hata hivyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumain Kweka aliiomba Mahakama kutoa adhabu kulingana na matakwa ya sheria ili iwe fundisho kwa watu wote ambao wanakwenda kinyume na majukumu waliyopewa.


Baada ya kusomewa hukumu hiyo, Mgonja aliondoka mapema katika eneo la Mahakama, Mramba na Yona wao wakiwa chini ya ulinzi walipelekwa eneo la chini na walionekana wakizungumza na ndugu na jamaa zao, akiwamo aliyekuwa Balozi wa Italia, Profesa Costa Mahalu wakati wakisubiri kupelekwa gerezani.


Wakati wote huo, ndugu na jamaa za washtakiwa hao walikuwa katika makundi wakijadiliana huku wengine wakitokwa na machozi.


Ilipofika saa 9.55 alasiri, Mramba na Yona walipandishwa katika ya gari aina ya Toyota Land Cruiser kupelekwa katika Gereza la Keko, chini ya ulinzi wa askari sita waliovalia kiraia wakiwa na silaha na wawili waliokuwa wamevalia sare za polisi.


Kabla ya kupandishwa ndani ya gari hilo, ndugu zao walipandisha ndoo mbili za rangi ya kijani ambazo zilikuwa na vitu ndani ambavyo havikufahamika, vikiaminika ni kwa ajili ya matumizi ya viongozi hao.


Jopo la mahakimu watatu waliokuwa wakiisikiliza kesi hiyo ni John Utamwa, Sam Rumanyika na Saul Kinemela.


Kabla ya kusomwa kwa hukumu hiyo, Utamwa aliarifu kuwa kulikuwapo na hukumu zilizotofautiana katika jopo hilo, hukumu ya wengi iliyosomwa na kuwatia hatiani washtakiwa hao na hukumu ya mmoja ambayo haikusomwa.


Kwa mujibu wa kesi hiyo iliyofunguliwa mwaka 2008, washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kuisababishia Serikali hasara ya kiasi hicho cha fedha kwa kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya M/S Alex Stewart ya Uingereza.


Utetezi
Katika utetezi wa Mgonja, alidai kuwa yeye ndiye aliyemshauri waziri wake zamani wa Fedha, Mramba kuisamehe kodi kampuni hiyo Oktoba 10, 2003 kwa sababu kulikuwa na mkataba uliosainiwa Juni 2003 kati ya kampuni hiyo na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambao ulikuwa unaonyesha malipo yafanyike bila ya kukatwa kodi.


Hata hivyo, ilidaiwa kuwa alitoa ushauri huo wakati wizara ilikuwa imekwishapata barua za Juni 24, 2003 na Oktoba 7, 2003 kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambazo zilikuwa zinakataza kampuni hiyo isisamehewe kodi.


Akijitetea, Mramba alidai kuwa kwenye kifungu cha 4.3.1 kilichopo kwenye mkataba huo ulioingiwa kati ya BoT na Alex Stewart Government Business Assayers kinasema malipo yoyote yatakayolipwa na mkataba huo hayatatozwa kodi. 


Hivyo alichokifanya ni kutekeleza matakwa ya mkataba huo kwa sababu Waziri wa Fedha pekee ndiye mwenye mamlaka ya kutekeleza mkataba huo.


Katika utetezi wa Yona, alidai kuwa mchakato wa kumpata mkaguzi wa madini ya dhahabu ulifuata utaratibu zote na kusimamiwa na Gavana wa BoT.


Alidai kuwa mwaka 2002 kulikuwa na malalamiko mengi kuhusu mapato ya dhahabu iliyokuwa ikichimbwa na kampuni tano za kigeni na kwamba wizara iliamua kuhakiki gharama za madini hayo.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: