
Na Mussa Ally BwakilaWahenga wa Uluguru, kuwasahau siwezi
Moro waloinusuru, awahifadhi Mwenyezi
Kupigania Uhuru, kuviokoa vizazi
Bwakila siwasahau, Wahenga wa Uluguru…
Machifu na Sultani, siwasahau ‘Wandewa’
Walotamba milimani, yasiyokuwa yakawa
Tutoe zawadi gani, kuenzi wazee hawa?
Bwakila siwasahau, Wahenga wa Uluguru…
Bambalawe na Kunambi , waloishika Matombo
Hawakuwa na vitimbi, ‘mambo yakawa si mambo’!
Bali walipiga kambi, hali isiende Kombo
Bwakila siwasahau, Wahenga wa Uluguru…
Msumi wetu Kibungo, ni Chifu wa kusifika
Pia Sultan Kingo, Kingoruwila kawika
Kingaru kaacha pengo, Ukami alikoshika
Bwakila siwasahau, Wahenga wa Uluguru…
Yupo Sultan Sabu, Mbilikila na Magoma
Viongozi wa ajabu, wenye hadhi na heshima
Kwa kweli sioni taabu, ya kuwapa sifa njema
Bwakila siwasahau, Wahenga wa Uluguru…
Yuko Mbago wa Mgeta, alowajenga ‘Wamwenda’
Bwakila nampa “Ngeta”, ujinga aliushinda
Elimu aloileta, Uluguru yawalinda
Bwakila siwasahau, Wahenga wa Uluguru…
Na Mdeng’o wa Magadu, yana ajabu mamboye
“Mkoloni ni mdudu, haifai kuwa naye”
“Kama mzoga kibudu”, hiyo ndiyo kauliye
Bwakila siwasahau, Wahenga wa Uluguru…
Kwa Lugege wa Mzinga, Mlapakolo na Hega
Karata walizichanga, Ubeberu kuupiga
Ukoloni walipinga, hawakusugua gaga
Bwakila siwasahau, Wahenga wa Uluguru…
Naye Lukwele wa Choma, sijui nimpe kombe?
Kuendeleza milima, Uluguruni watambe!
Vitani alojitoma, kaitwa “Mdima Ng’ombe”
Bwakila siwasahau, Wahenga wa Uluguru…
Dendego wa Tegetero, mpambanaji shupavu
Wala hakuona kero, kwa TANU kuipa nguvu
Fahari ya Morogoro, kwa akilize angavu
Bwakila siwasahau, Wahenga wa Uluguru…
Aidha Sharifu Dosi, simsahau na Mwene
Hao wote waasisi, Uhuru upatikane
Sasa bila wasiwasi, “Nilongele Mkagone”…
Bwakila siwasahau, Wahenga wa Uluguru…
Wapo wengi na wengine, orodha yao ni ndefu
Naapa siku nyingine, nayo nitaidurufu
Ya kwao yaonekane, walofanya Matukufu
Bwakila siwasahau, Wahenga wa Uluguru…
Hao viongozi bora, sio bora viongozi
Waliona ni hasara, kukosa kitu Azizi
Wakafanya barabara, ya Uhuru iwe wazi
Bwakila siwasahau, Wahenga wa Uluguru…
Mussa A.S Bwakila Lukwele Msumi.
Walotamba milimani, yasiyokuwa yakawa
Tutoe zawadi gani, kuenzi wazee hawa?
Bwakila siwasahau, Wahenga wa Uluguru…
Bambalawe na Kunambi , waloishika Matombo
Hawakuwa na vitimbi, ‘mambo yakawa si mambo’!
Bali walipiga kambi, hali isiende Kombo
Bwakila siwasahau, Wahenga wa Uluguru…
Msumi wetu Kibungo, ni Chifu wa kusifika
Pia Sultan Kingo, Kingoruwila kawika
Kingaru kaacha pengo, Ukami alikoshika
Bwakila siwasahau, Wahenga wa Uluguru…
Yupo Sultan Sabu, Mbilikila na Magoma
Viongozi wa ajabu, wenye hadhi na heshima
Kwa kweli sioni taabu, ya kuwapa sifa njema
Bwakila siwasahau, Wahenga wa Uluguru…
Yuko Mbago wa Mgeta, alowajenga ‘Wamwenda’
Bwakila nampa “Ngeta”, ujinga aliushinda
Elimu aloileta, Uluguru yawalinda
Bwakila siwasahau, Wahenga wa Uluguru…
Na Mdeng’o wa Magadu, yana ajabu mamboye
“Mkoloni ni mdudu, haifai kuwa naye”
“Kama mzoga kibudu”, hiyo ndiyo kauliye
Bwakila siwasahau, Wahenga wa Uluguru…
Kwa Lugege wa Mzinga, Mlapakolo na Hega
Karata walizichanga, Ubeberu kuupiga
Ukoloni walipinga, hawakusugua gaga
Bwakila siwasahau, Wahenga wa Uluguru…
Naye Lukwele wa Choma, sijui nimpe kombe?
Kuendeleza milima, Uluguruni watambe!
Vitani alojitoma, kaitwa “Mdima Ng’ombe”
Bwakila siwasahau, Wahenga wa Uluguru…
Dendego wa Tegetero, mpambanaji shupavu
Wala hakuona kero, kwa TANU kuipa nguvu
Fahari ya Morogoro, kwa akilize angavu
Bwakila siwasahau, Wahenga wa Uluguru…
Aidha Sharifu Dosi, simsahau na Mwene
Hao wote waasisi, Uhuru upatikane
Sasa bila wasiwasi, “Nilongele Mkagone”…
Bwakila siwasahau, Wahenga wa Uluguru…
Wapo wengi na wengine, orodha yao ni ndefu
Naapa siku nyingine, nayo nitaidurufu
Ya kwao yaonekane, walofanya Matukufu
Bwakila siwasahau, Wahenga wa Uluguru…
Hao viongozi bora, sio bora viongozi
Waliona ni hasara, kukosa kitu Azizi
Wakafanya barabara, ya Uhuru iwe wazi
Bwakila siwasahau, Wahenga wa Uluguru…
Mussa A.S Bwakila Lukwele Msumi.

0 comments:
Post a Comment