BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BINTI WA MIAKA 11 AJIFUNGUA MTOTO WA KIKE BAADA YA KUSHIKA MIMBA.

PICHA YA MTOTO KUTOKA MAKTABA.

Binti wa miaka kumi na mmoja nchini Paraguay aliyedai kubakwa na baba yake wa kambo amejifungua mtoto wa kike baada ya mamlaka nchini humo kumzuia asitoe ujauzito aliokua nao.

Madaktari katika mji mkuu wa Asuncion wamesema binti huyo na mtoto wake aliyejifungua kwa njia ya upasuaji wanaendelea vizuri.

 
Kampeni imeanzishwa kupinga ubakaji kwasababu ya kisa cha binti huyo.
 
Tukio hilo limesababisha utata mkubwa nchini Paraguay na katika mitandao ya kijamii, Paraguay ni taifa linaloamini zaidi katika Ukatoliki ambapo mwanamke anaruhusiwa kutoa mimba pale tu afya yake inapokuwa hatarini.

Binti huyo alibakwa alipokua na umri wa miaka kumi pekee na Baba yake wa kambo mwenye miaka arobaini na miwili yupo rumande akisubiria kutajwa kwa kesi yake wakati huo huo baba huyo amekanusha kuhusika katika tukio hilo.bbc
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: