BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NDEGE YA SHIRIKA LA TRIGANA AIR YAPOTEA BAADA YA KURUKA ANGANI IKIWA NA ABIRIA 54 WAKIWEMO NA WATOTO WATANO.

http://media.viva.co.id/thumbs2/2010/12/27/102168_trigana-air-lepas-landas--take-off--di-bandara-supadio--pontianak_663_382.jpg
Mamlaka nchini Indonessia inasema kuwa ndege moja ya abiria iliowabeba watu 54 wakiwemo watoto watano imepoteza mawasiliano na idara ya kituo cha udhibiti safari za ndege.

Maafisa wa idara ya uchukuzi wanasema kuwa ndege hiyo inayomilikiwa na huduma ya Trigana Air ililikuwa ikielekea katika mji wa Oksibil mashambani, mashariki mwa jimbo la Papua kabla ya kutoweka. Papua

Msemaji wa wizara hiyo amesema kuwa hatua za kuisaka ndege hiyo zimeanza na zinashirikisha mamlaka ya eneo hilo na kwamba hali mbaya ya hewa katika milima ya eneo hilo inaathiri harakati hizo.

Waandishi wanasema kuwa taifa la Indonesia lina rekodi mbaya ya ajali za ndege huku ajali mbili zikiwa tayari zimeripotiwa mwaka mmoja ulioipita. Milima ya papua

Ndege ya Indonesia Air ilianguka katika bahari ya Java mwezi Disemba ilipokuwa ikitoka Sura Baya kuelekea Singapore na hivyobasi kuwaua watu wote 192 walioabiri chombo hicho.

Vilevile ndege moja ya kijeshi ilianguka katika makaazi ya watu huko Medan Sumatra mnamo mwezi Julai na kuwaua zaidi ya watu 140 ikiwemo watu kadhaa ardhini.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: