BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NG'OMBE AUA WATU SABA BAADA YA KUWAKUMBA NA PEMBE.

Ng'ombe wanaotumiwa katika mchezo wa Matador wamewaua watu saba katika sherehe nchini Uhispania tangu mwanzo wa mwezi Julai huku wanne wakiuawa wikendi iliopita.Vifo hivyo vilitokea wakati wa kufukuzana na ng'ombe hao katika barabara na sio ndani ya ukumbi wa mchezo huo.
https://coupeaunoir.files.wordpress.com/2010/10/image-6-for-matadors-being-gored-by-bulls-gallery-5473956681.jpgNi idadi kubwa ya vifo iliorekodiwa katika mda mfupi.
Miongoni mwa waliouawa ni diwani mmoja mwenye umri wa miaka 36 aliyeuawa katika mji wa Penafiel,mji ulio karibu na ule wa Valladolid kaskazini mwa Madrid.

Kaskazini zaidi kijana mwenye umri wa miaka 18 alidungwa kwenye tumbo na ng'ombe na kufariki katika eneo la Lerin huko Navarra.

Vifo vyengine vilitokea wakati wa sherehe za ngombe katika majimbo ya Valencia,Murcia,Toledo,Castellon na Alicante.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: