BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

OLE SENDEKA AMCHAMBA FREDIRICK SUMAYE KWA KUONYESHA UDHAIFA WA KUIHAMA CCM NA KUINGIA UKAWA KISHA KULA MATAPISHI YAKE.


Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye (Kulia) akiwa na Mgombea urais kupitia Chadema Edward Lowassa.

Manyara.
Mgombea ubunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka amesema Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye ameonyesha udhaifu kisiasa kwa kuhamia upinzani kwa kuwa aliapiza Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa akipitishwa anahama chama.

Akizungumza kwenye mkutano wa kumwaga sera za CCM za Mgombea Mwenza, Samia Suluhu Hassan, Ole Sendeka alisema ameshangazwa na uamuzi huo na kwanza Sumaye amekula matapishi yake.

“Sumaye kujitoa CCM na kuhamia Ukawa ameonyesha udhaifu mkubwa si alidai kwamba endapo CCM itampitisha, Lowassa kugombea urais atakihama chama.

“Huyu huyu alisema Lowassa hafai kuwaongoza na kuwatumikia Watanzania, cha ajabu juzi amekula matapishi yake,” alifafanua Sendeka

Sendeka ambaye alipitishwa kwa kura nyingi Simanjiro, alisema wagombea wa vyama vya siasa kwa nafasi zao wanatakiwa kutumia lugha za kistaarabu na kunadi sera zao majukwaani.

Ole Sendeka alisema kuwa ustaarabu wa kisiasa ni pamoja na kuwaeleza watu sifa za mgombea wa chama kingine ili wajue sifa alizonazo.

Alieleza kwamba kutokana na tabia walizozionyesha baadhi ya wagombea na wanachama waliotoka CCM na kujiunga na vyama vya upinzani kwa kubadili uhalisia wao na mpaka wa makabila ili kujipatia kura.

“Mimi ni mtu lakini mwenye kabila langu Maasai, na dini yangu ni Mkristo Mluteri nitaenda kuomba kwa Wakatoliki au Waislamu huku wakijua dini yangu na kabila langu, siwezi kwenda nikawaambia wanisilimishe lakini Lowassa alikuwa CCM na ili apate kura nyingi aliwakataa ndugu zake Wameru na kusema ni Maasai” alisema Ole Sendeka.

Aidha alifafanua kwamba chama cha siasa kinaundwa na watu na itikadi moja na hakiwezi kuuzwa kama Kampuni na kuongeza kuwa chama kimoja cha upinzani kimeuzwa kwabei ndogo kutokana na aliyekinunua kuwa na uchu wa madaraka ya kukalia kiti cha Urais.

Naye Mgombea Mwenza Samia Suluhu Hassan aliwaomba Wananchi wa mkoa wa Manyara kuipa CCM ushindi ili wawaeze kuwatumikia na kutatua matatizo yao yanayowakabili ambayo hayajatekelezeka kwa kipindi kilichopita.

“Kama mtatupa kura mambo tutakayowafanyia ni pamoja na kuwatatulia migogoro ya ardhi iliyopo, na kuwarudishia maeneo yaliyotwaliwa na wawekezaji pia nitasimamia tatizo la akina mama wajawazito na watoto na kulisimamaia kikamilifu suala la huduma ya afya,” alieleza mgombea huyo. CHANZO:MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: