WAFUGAJI SASA WAPIGWA MARUFUKU MTO MALAGARASI KIGOMA.
Uvinza. Wafugaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Mkoa wa Kigoma, wametakiwa kuacha tabia ya kuogesha mifugo katika vyanzo vya maji vilivyopo kwenye halmashauri hiyo, hususani Mto Malagarasi ili kutunza vyanzo hivyo.
Hayo yalielezwa na Donald Kasongi kutoka tafiti ya mazingira katika mafunzo ya wadau wa mazingira baada ya kubaini kuwa wafugaji wengi, hutumia dawa za kuogesha mifugo kwenye vyanzo vya maji ukiwemo Mto Malagarasi ambao ni chanzo kikubwa cha matumizi ya jamii inayoishi pembezoni mwa mto huo.
Wakitoa malalamiko hayo baadhi ya wadau wa mazingira, Hemid Kisobwe na Emmanuel Kipanti kwa nyakati tofauti walisema, changamoto kubwa inatokana na wahusika kwa kushindwa kudhibiti, kulinda na kuchukua hatua kamili kwa wahalifu wa mazingira kwa mujibu wa mafunzo elekezi ya kinga na tahadhari, waliyopewa na wadau na watafiti wa mazingira ni muhimu kulinda vyanzo vya maji.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa halmashauri ya Uvinza Ofisa Misitu, Emily Gwejo alikiri kuwepo kwa changamoto hizo, na kudai kuwa hali hiyo inachangiwa na uhaba wa fedha za kufanya doria na posho za walinzi hali inayokwamisha shughuli mbali mbali.CHANZO:MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment