BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

PETER MSIGWA WA CHADEMA AKOSA FURHA KUTOKANA NA TAARIFA ZA KUPEWA FEDHA SH200 MIL ZA KUSOMBA WATU ILI WAJAE KATIKA MKUTANO WA KAMPENI WA EDWARD LOWASSA LEO IRINGA.

 
Mgombea ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Peter Msigwa, amesema hatavumilia propaganda zinazosambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ya kumchafua yeye na mgombea urais kupitia chama hicho, Edward Lowassa.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Msigwa alisema kuwa kuna watu wanaozusha kwenye mitandao ya kijamii kuwa amepewa pesa za kununua watu ili waweze kufika kwenye mkutano wa Chadema utakaofanyika leo mjini hapa.

Nasikitika kwa yaliyotolewa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa mimi nimepewa milioni 200 kwa ajili ya kufanya maandalizi ya kununua, kusomba, kuwapatia madereva bodaboda ili waweze kufika kwenye mkutano wa hadhara wa Edward Lowassa utakaofanyika siku ya Jumapili Agosti 30, alisema.

Ni dhahiri kuwa maneno hayo yaliandikwa pengine na watu wanaotumiwa na wapinzani wangu kufifisha hali na moyo wa kujitolea kwa viongozi wa chama, wafuasi na wananchi na wapiga kura wetu wa jimbo la Iringa mjini, alisema Msigwa.

Aidha, alisema Chadema hakijawahi wala hakina mpango wa kusomba wananchi au kutoa fedha ili wahudhurie mikutano yao bali chama hicho kimekuwa kikichangiwa fedha na wananchi na wamekua wakijitolea bila kulipwa hata senti tano.

Alisema kuwa chama hicho kimejipanga kufanya kampeni za kistaarabu zisizo na matusi na zinalenga na kujikita kwenye kuendeleza na kuwaambia wananchi ni kitu gani kinatakiwa kufanyika ili waweze kuondokana na umasikini na ndio imekuwa hoja yake kwa wananchi.

Alisema kuwa kwa sasa Chadema kimeshashinda na mbinu pekee waliyobaki nayo CCM ni kutaka kufanya kampeni chafu za kukichafua chama hicho na kilitahadharisha jeshi la polisi kuchukua hatua pindi watakapoona vurugu.

Alisema kuwa jimbo la Iringa Mjini litazindua kampeni zao rasmi Septemba 12 ili kueleza wananchi sera na dira ya jimbo la Iringa na taifa kwa ujumla.

Alisema kuwa jimbo la Iringa mjini limepewa fursa kubwa ya kutembelea na mgombea urais atawahutubia wananchi wa mkoa huo.

Alisema Lowassa ataanza kuhutubia wananchi wa Ilula, Mafinga, Pawaga, Kalenga na baadaye Jimbo la Iringa Mjini.CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: