BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

JANUARI MAKAMBA AELEZA UDHAIFU WA MGOMBEA URAIS WA UKAWA EDWARD LOWASSA.

Dodoma. Aliyekuwa mgombea Urais wa CCM ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, Januari Makamba, jana alimshukia mgombea urais kwa tiketi ya Ukawa, Edward Lowassa kwamba ni mroho wa madaraka.

Makamba alitoa kauli hiyo katika viwanja vya Barafu mjini Dodoma wakati akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde. 


January alisema kuwa Lowassa ameivuruga demokrasia ndani ya Chadema na kupeleka mizengwe itakayokiua chama hicho na umoja wao.

“Yale siyo mabadiliko kama wanavyojinadi bali ni uroho wa madaraka kwa mtu mwenye uroho na chama chenye uroho, lakini hawezi na hawawezi kushika madaraka ya kuongoza nchi,” alisema Makamba.

Alisema kinachoendelea kwa vyama vinavyounda Ukawa ni maigizo na siyo mabadiliko ya kweli kwa sababu mgombea urais ametoka CCM na Sera za CCM na mgombea mwenza ametoka CUF na sera za huko, hivyo hawawezi kuungana kwa pamoja kwa sababu hawajui nini maana ya kile wanachogombea.

Hata hivyo, Makamba alikiri kuwa uchaguzi wa mwaka huu ni mgumu kuliko uchaguzi wowote uliowahi kutokea katika mfumo wa vyama vingi na akawataka wana CCM kujiandaa kikamilifu.

Alisema CCM kinapaswa kuwa makini na imara wakati wote ili kutoyumba na wakifanya hivyo watajikuta wanapata mchanganyiko ambao utaleta shida katika maendeleo.

Kwa upande wake mgombea ubunge Mavunde alijipachika jina la Mr Makao akisema lazima ataipelekea Dodoma hadhi ya kweli katika kufikia makao ambayo yamekuwa yakisemwa kama hisani. 


Mavunde aliomba wananchi kumwamini na kumpa nafasi hiyo kwani ana uhakika kwa miaka mitano ataifanya Dodoma kupaa kiuchumi huku akisema atashughulika na watu wenye kipato cha chini pamoja na kumaliza migogoro ya ardhi.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: