Katibu Mkuu Mtendaji wa chama cha soka wilaya ya Morogoro (MMFA) Kafare Maharagande kushoto akitumbukiza karatasi baada ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa chama cha soka mkoa wa Morogoro uliofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya Manispaa hiyo mwishoni mwa juma, Picha na Juma Mtanda.
Na Juma Mtanda, Morogoro.
Chama cha soka mkoa wa Morogoro kimepata viongozi wapya katika nafasi mbalimbali huku nafasi ya Katibu Mkuu Mtendaji kukijitokeza upinzani mkubwa baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa kuchagua viongozi wa chama hicho uliofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya Manispaa ya Morogoro jana.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi wa chama cha soka mkoa wa Morogoro (MFRA), Alex Sikalumba alieleza kuwa katika uchaguzi huo ulikuwa na ushindani hasa katika nafasi ya Katibu Mkuu Mtendaji hali iliyofanya kamati yake irudie uchaguzi katika nafasi hiyo.
Sikalumba alisema kuwa katika nafasi hiyo hivyo Mwakambaya na Kimbawala ndio wataorudia kwa kupigiwa kura ili atatikane mshindi.”alisema Sikalumba.
Baada ya kurudia uchaguzi huo, Charles Mwakambaya alifanikiwa kumdondosha Emmanuel Kimbawala kwa kura 16 dhidi ya 15.
Katika nafasi ya Mwenyekiti wa chama hicho, Pascol Kihanga alifanikiwa kurudi tena madarakani baada ya kumbwaga mpinzani wake Erinest Mlinda kwa kupata kura 24 kwa kura nane baada ya kupigwa kura halali 32 huku kura moja iliharibika.
Kwa upande wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti walijitokeza wagombea wanne kura huku Gracian Makota akiibuka kidedea kwa kupata kura 21 na kufuatiwa na Robert Selasela aliyepata kura tisa, Tito Haule kura tatu na Juma Mganga Masine aliyepata kura 0.
Katibu Mkuu Mtendaji, katika nafasi hii uchaguzi ulirudiwa baada ya wagombea wanne kushindwa kumpata mshindi na wagombea wawili walirudia uchagzi, Emmanue Kimbawala kura 15 na Charles Mwakambaya aliyepata kura 16.
Katibu Mkuu Msaidizi wagombea wawili, Jimmy Lengwe alipata kura 18 baada ya kumshinda Beatrice Fakihi aliyepata kura 15.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa katika nafasi ya Mweka Hazina lilijitokeza jina la mgombea mmoja, Peter Mshigati aliyepigiwa kura 30 huku wajumbe watatu wakimkataa huku
Mjumbe Mkutano Mkuu wa TFF, Hassan Masoud Mamba (Bantu) akipita bila kupingwa katika uchaguzi huo kwa kupigiwa kura za ndiyo 33.
Katika nafasi ya Mwakilishi wa Vilabu walijitokeza wagombea wawili huku, Ramadhan Mnyolole (Wagala) akimbwaga mwandishi, Nickson Mkilanywa kwa kura 21 dhidi ya kura 12
Upande wa nafasi ya Kamati Tendaji walijitokeza wagombea sita huku majina matatu yakipenya kwenye orosha hiyo ikiongozwa na Mrisho Javu aliyepata kura 25, Rajabu Kiwanga kura 22 na Boniface Kiwale 17 wakati Mhandisi Bahati Mwaseba alipata kura saba, Salum Mshauri Nasouro kura 12, Clement Bazo 16.

0 comments:
Post a Comment