BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CCM NAMNA WALIVYOZINDUA KAMPENI ZA UBUNGE NA UDIWANI MANISPAA YA MOROGORO.

 
Mkazi wa Manispaa ya Morogoro akifuatilia matukio ya uzinduzi wa kampeni ya CCM ya udiwani na Ubunge katika uwanja wa Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro.
Mgombea ubunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Mohamed Abood akizungumza na wananchi wakati akiomba kura katika uzinduzi wa kampeni ya chama cha mapinduzi (CCM) katika mkutano uliofanyika uwanja wa Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Morogoro, Fikiri Juma akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Morogoro mjini kupitia chama hicho, Abdullaziz Abood wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu katika uwanja wa Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro jana.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Morogoro, Fikiri Juma na mgombea ubunge wa jimbo hilo la Morogoro mjini, Abdullaziz Abood wakimnadi mgombea urais ndani ya CCM kupitia wakati wa mkutano huo.

Mgombea ubunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Mohamed Abood kulia akiwa na wagombea udiwani wa kata 29 huku wakinyanyua vitabu vya ilani ya utekelezaji ya mwaka 2015-2020 ya chama cha mapinduzi (CCM) wakati wa uzinduzi wa kampeni ya chama hicho katika uwanja wa Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro.
Diwani wa kata ya Mjimkuu Hassan Malingo akipata msaada wa kushuka katika jukwaa mara baada ya kukabidhiwa ilani ya chama hicho.
Huyu pia ni mgombea udiwani wa kata ya Mbuyuni Samuel Msuya naye akishuka katika jukwaa hilo mara baada ya kukabidhiwa ilani ya chama hicho ambapo CCM imesimamisha jumla ya wagombea udiwani katika kata 29 zinazounda Manispaa ya Morogoro.
Sehemu ya wanaCCM na wananchi wengine wakifuatilia matukio ya mkutano huo


Wakila kiapo
Mgombea udiwani kata ya Sabasaba Mudhihil Shoo akitambulisha wakati wa utambulisho wa madiwani katika ufunguzi wa kampeni hiyo.
Aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Morogoro na mgombea udiwani kata ya Boma, Amir Juma Nondo akizungumza jambo wakati wa ufunguzi huo, kushoto ni Katibu wa CCM wilaya ya Manispaa, Kulwa Milonge na kulia ni mgombea ubunge jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Abood.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: