BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DK SLAA ASUBIRI KWA HAMU RUNGU LA ASKOFU GWAJIMA BAADA YA KUITWA MSHENGA WA EDWARD LOWASSA CHADEMA.

Aliyekuwa Katibu wa Chama cha Demokrasia na
Aliyekuwa Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa. 


Dar es Salaam.
Aliyekuwa Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa amesema anasubiri kwa hamu kujibiwa na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kama alivyotangaza kanisani kwake Jumapili iliyopita.

Akiwa kanisani hapo juzi, Askofu Gwajima alikaririwa akisema atajibu mapigo kuhusu tuhuma zilizotolewa dhidi yake na Dk Slaa katika hotuba yake ya Septemba Mosi.

Katika hotuba hiyo, Dk Slaa alimwita kiongozi huyo wa Kiroho kuwa ni mshenga wa Edward Lowassa kwa Chadema.

Mwanasiasa huyo mstaafu alizungumza kwenye Hoteli ya Serena baada ya kutoelewana na viongozi wenzake wa Chadema kumpokea Lowassa ajiunge na chama hicho.

“Ukweli unasemwa kama ulivyo, hauyumbishwi yumbishwi, kama anataka kukanusha au kujibu chochote basi afanye hivyo,” alisema Dk Slaa.

Alisema anamshangaa Askofu Gwajima alipohojiwa na gazeti hili baada ya hotuba yake alikanusha kuwa mshenga hali akijua kuwa alizungumza naye (Dk Slaa) wakiwa pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, mke wake, Josephine Mushumbusi na baadhi ya viongozi wa chama hicho.

“Ninachosema kama hana hofu ya Mungu aendelee na akitaka kukanusha au kujibu mapigo ajibu,” alisema.

Hata hivyo, Dk Slaa alikanusha kuwatuhumu maaskofu 30 kati ya 34 kupewa fedha na badala yake alisema alikuwa ananukuu kile alichosema Gwajima katika kikao kilichofanyika Julai 27.

“Askofu Gwajima alisema hayo wakati akinishawishi nimkubali Lowassa nikiwa nyumbani kwangu Julai 28,” alisema Dk Slaa.

Pia, alikanusha kumtuhumu Rostam Aziz kutoa kiasi cha Sh15 bilioni kwa ajili ya kampeni badala yake alisema maneno hayo yalitamkwa na Askofu Gwajima mwenyewe. MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: