BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

JAMHURI YA WATU WA CHINA WATOA MISAADA YA KIJAMII WILAYA YA KILOSA MOROGORO.

Balozi msaidizi wa jamhuri ya watu wa China,  Zang Biao akikabidhi sehemu ya vifaa ikiwemo mipira kwa wanafunzi wa shule ya msingi Mvumi wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro. Picha na Joseph Malembeka)

Balozi msaidizi wa Jamhuri ya watu wa China, Zang Biao kati kati ya wanafunzi wawili ishara ya kukabidhi madawato 80 katika shule ya msingi ya Mvumi na Chagongwe huku nyuma kukiwa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo, John Henjewele.

Mkuu wa wilya Kilosa John Henjewele akihutubia katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Mil.24 vikiwemo vifaa vya shule na kilimo kwa lengo la kuondoa umasikini wilaya ya Kilosa.
Balozi Msaidizi wa Jamhuri ya watu wa China, Zang Biao akiitazama sanamu ya mwanamke wa kiafrika muda mufupi baada ya kukabidhiwa kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Kilosa, John Henjewele ikiwa ni kumbukumbu na ishara ya kuhusiano baina ya nchi hiyo katika kijiji cha Peapea kilichopo wilayani humo mkoani Morogoro.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: