BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MKUTANO WA KAMPENI WA DK MAGUFULI WALETA MAAFA MOROGORO, WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA KATIKA MKANYAGANO UWANJA WA JAMHURI.

mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli akiwahutubia wakazi wa mkoa wa Morogoro katika mkutano wa kampeni uwanja wa jamhuri Morogoro.Picha na Juma Mtanda.

Watu wawili wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa kutokana na mkanyagano uliotokea jana Uwanja wa Jamhuri, Morogoro katika mkutano wa kampeni za mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli.

Tayari leo, Mwenyekiti wa CCM taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amewatembelea majeruhi hao waliolazwa Hospitali ya Mkoa Morogoro.

Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk Ritha Lyamuya amesema walipokea watu 19 waliokuwa na majeraha yakiwemo ya kuvunjika maeneo mbalimbali ya mwili na kuongeza kuwa miongoni mwao, wawili walikufa kutokana na kuumia vibaya.

Aidha Dk Lyamuya alisema kuwa wagonjwa ambao bado wamelazwa wako 10 na wengine saba walitibiwa na kuruhusiwa.

Dk Lyamuya alisema kuwa waliokufa ni pamoja na mwanamke anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 42 na mtoto wa umri wa miaka 12 aliyejulikana kwa jina la Ramadhan Abdalah.

Uwanja wa Jamhuri jana ulifurika watu wakati mgombea urais kwa tiketi ya CCM John Magufuli alipokwenda kwa ajili ya kufanya kampeni.

Mara tu baada ya Magufuli na viongozi wengine kuondoka uwanjani hapo, ndipo hali ya kusukumana na kukanyagana ilitokea getini wakati watu wakitoka.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: