BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS KIKWETE ASABABISHA MGOMBEA URAIS KUANGUA KILIO KATIKA MKUTANO WA KAMPENI UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 25.


Mgombea Urais kupitia Chama cha CHAUMMA Mhe Mohammed Masoud Rashid akiwahutubia wananchi wakati wa mkutano wake wa kampeni


 Mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha Chauma, Mohammed Masod Rashid, amejikuta akiangua kilio jukwaani na kumpigia magoti Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, kumuomba awaachie huru masheikh wa Jumuiya ya Mihadhara ya Dini ya Kiislamu (Uamsho) waliopo gerezani.

Tukio hilo lilitokea katika mkutano wa hadhara wakati akifungua kampeni za chama hicho visiwani hapa.

Mgombea huyo alivuta hisia za wananchi na kila aliyekuwa akipita njia katika eneo hilo la kiwanja cha Komba Wapya kilichopo mjini hapa kusitisha safari yake na kuanza kumsikiliza wakati akiangua kilio.

Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe Mohammed Masoud Rashid akionesha mkoba wake uliokuwa na fomu ya kuwania urais wa Zanzibar hivi karibuni.

Mgombea huyo aliacha kunadi sera na kuangua kilio akiwalilia masheikh hao wanaokabiliwa na kesi ya kusaidia ugaidi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Nakupigia magoti Rais Kikwete naomba uwatoe masheikh wetu kwani unawavunjia haki zao za msingi, alisema mgombea huyo wa urais.

Alisema endapo atapata ridhaa ya Wazanzibari kuwa rais atatoa msamaha kwa wafungwa walioko gerezani ambao wanamakosa madogo madogo.SOURCE: NIPASHE
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: