BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TEKNOLOJIA YA INTERNET YAPORA RASMI MALEZI BORA YA WATOTO, ANALOJIA YAPIGWA TEKE.


WAZAZI makini na wenye uchungu na maisha ya baadaye ya watoto wao, watakubaliana na safu hii kwamba wanahitaji nguvu ya ziada katika makuzi na malezi ya watoto wao wa kizazi hiki cha dijitali ambacho ndiyo kwanza kimeanza kupamba moto kutupilia mbali mfumo wa analojia uliotulea sisi wazazi wao.

Hiki ni kizazi cha matumizi mkubwa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) kupitia kompyuta, simu za mkononi, mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na barua pepe, tovuti, facebook, YouTube na mingine mingi.

Tofauti na wakati wa analojia ambapo ili kuwasiliana tulihitaji kuandikiana barua, kutumia telegramu za ujumbe mfupi au fedha kwa njia ya mitandao ya posta au kwa njia ya simu zilizounganishwa nyaya na kuchukua muda mrefu kabla ya mhusika kupata ujumbe.

Hali hiyo sasa inaendelea kukaribia kuwa historia kwa maana ya matumizi yake yanazidi kupungua kutokana na uvumbuzi na maendeleo ya ICT. Mawasiliano sasa yapo kiganjani mwako.

Unachohitaji ni kuwa na simu yako ya mkononi yenye uwezo wa kupokea huduma hizo mara moja kutoka mahali ulipo mradi mahali hapo pawe ni mtandao unauwezesha kukuunganisha na wengine mahali popote.

Unaweza kusikikia redio, kushuhudia matukio yanayotangazwa moja kwa moja na televisheni na redio mahali popote duniani au hata kusoma magazeti kwenye mitandao bila kulazimika kwenda kulinunua mahali. Mawasiliano ya dijitali yanavuka mipaka ya nchi na mabara duniani.

Unatuma ujumbe sasa hivi kwa kutumia mitandao na katika kipindi cha karibu chini ya dakika moja mamia, maelfu na pingine mamilioni ya watu wanaweza kushuhudia duniani. Lakini urahisi huu wa mawasiliano sasa nao umekuja na mfumo hasi pia katika suala zima la malezi ya watoto.

Udhibiti wa mienendoni yao, au aina ya taarifa wanazotafuta kupitia mitandaoni na picha au matukio wanayostahili kuyaona watoto wa chini ya miaka 18 sasa yanaelekea kuwa ndoto za mchana kuweza kuyadhibiti. 


Watoto hivi sasa kwa kweli wako katika dunia ya utandawazi kiasi kwamba wazazi na walezi makini tupo katika njia panda.

Tufanyeje ili tuweze kurejesha angalau kwa kiasi fulani udhibiti wa tabia na maisha yao kama watoto, tena watoto wa kiafrika? Ni kama vile utandawazi umeshafikia hatua za kutuzidi nguvu wazazi na udhibiti wa tabia, hasa wanazojifunza watoto kupitia utandawazi.

Watoto wetu hata kama hatuwanunulii simu za kuweza kufanya mawasiliano wanayopenda, huweza kutumia simu za marafiki zao au kwenda kwenye vioski vya mitandao kubrauzi wenyewe na kujipatia picha za ajabu ajabu zikiwemo za ngono.

Zamani wakati wa analojia wazazi waliweza kutoka na watoto wao kwenda kwenye majumba ya sinema zinazoonesha picha ambazo watu wazima na watoto kwa pamoja wanaweza kuziona. Hivi sasa majumba hayo hayapo kwa wingi kama enzi hizo.

Utandawazi umeathiri na kuendelea kuathiri watoto wetu kwa kupitia simu za kiganjani, televisheni, muziki wa kizazi kipya, sinema za ngono na wala siyo mapenzi kiasi kwamba watoto wetu tumewajengea taswira kwamba dunia hii ni raha na starehe tupu.Tutafika kweli?HABARILEO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: