ZITTO: MAGUFULI
hajawahi kukemea
ufisadi
Akihojiwa na mtangazaji Tido Mhando katika
kipindi cha mikikimikiki AZAM 2 TV leo
asubuhi, Zitto ameshangazwa na hatua ya
mgombea urais kupitia CCM kujipambanua
kuuchukiaufisadi wakati kipindi chote cha
mijadala ya ufisadi wa EPA, MEREMETA,
BUZWAGI, TOKOMEZA, RICHMOND, ESCROW
nk hakuwahi kukemea lolote.
ZITTO alienda mbali zaidi kuhusiana na kauli
ya Magufuli hivi karibuni akiwa Tanga
kwamba atayarejesha mashamba ya mkonge
kwa wananchi ilihali yeye Zitto alileta hoja
hiyo ya mkonge bungeni na Magufuli
aliungana na wenzie kuipinga hoja hiyo kwa
macho makavu, leo anaudanganya umma
kuwa atayarejesha ni usanii mkubwa.
Chanzo: AZAM II TV

0 comments:
Post a Comment