BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HANIWEZI !!! DK JOHN MAGUFULI AKIMBIZA EDWARD LOWASSA UCHAGUZI MKUU 2015 MATOKEO YA URAIS.

Mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli.
Mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli.

WAKATI Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ikitarajia kutangaza mshindi wa kiti cha urais kesho, mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli anaongoza katika majimbo mengi, ambayo Tume imeyatangaza matokeo yake kuanzia juzi.

Katika majimbo 113 ambayo NEC chini ya Mwenyekiti wake, Jaji mstaafu Damian Lubuva iliyatangaza hadi kufikia jana saa tatu usiku, Dk Magufuli anaongoza katika majimbo 88 huku mpinzani wake, Edward Lowassa wa Chama cha Demokrasia na Mendeleo (Chadema) akiongoza katika majimbo 25.

Majimbo yapo 264. Kutokana na matokeo ambayo yametangazwa kwa siku ya pili, Magufuli amejikusanyika kura 2,485,506 dhidi ya kura 1,780,940 alizopata Lowassa, ikiwa ni tofauti ya kura 704,566.

Majimbo yaliyotangazwa jana usiku ni Mfenesini, Mahonda, Rungwe, Arumeru Magharibi, Pangani, Korogwe Vijijini, Kijito Upele, Chaani, Kiembesamaki, Manyoni, Iramba, Dimani, Nzega, Igunga, Urambo, Babati, Kiteto, Bukene, Sikonge, Kaliua, Bulyanhulu, Kyela, Manonga, Ukerewe, Mpwapwa, Longido na Kondoa Mjini.

Hata hivyo, mwelekeo wa ushindi kwa wagombea wa vyama vilivyokuwa na ushindani mkubwa yanaweza kuanza kuonesha mwelekeo baada ya kukamilika kwa matokeo ya mikoa kadhaa iliyokuwa na wapiga kura wengi waliojiandikisha na kuonekana kuwa ni ngome za vyama hivyo kama majimbo ya mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya, Morogoro, Tanga, Mara, Kagera, Tabora na Dodoma.

Uchaguzi Mkuu ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita na kuwashindanisha wagombea wanane, ambao ni mbali ya Dk Magufuli na Lowassa ni Anna Mghwira (ACT-Wazalendo), Chief Litayosa Yemba (ADC), Hashim Rungwe (CHAUMMA), Janken Kasambala (NRA), Lyimo Macmillan (TLP) na Fahmi Dovutwa (UPDP).

Awali, akizungumza na waandishi wa habari jana, Jaji Lubuva alisisitiza kuwa inatangaza matokeo kwa kadri inavyopokea na siyo kwa kupendelea upande wowote au kujali aliyeshinda au kwa matakwa ya vyama vya siasa.

Alisema tume hiyo inafanya kazi kwa kuzingatia taratibu na hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kuwapangia njia ya kutoa matokeo. Alisema madai yaliyotolewa na Chadema kuwa wanatangaza matokeo ya maeneo ambayo CCM imeshinda ili kuaminisha umma kuwa ni washindi siyo ya kweli.

“Wakati huu tusingependa kulumbana na chama au vyama vya siasa hata mgombea yeyote, matokeo tunayoyapokea ndiyo tunayatangaza, malalamiko ya kuwa NEC inatangaza kwa mwelekeo wa kupendelea siyo kweli, tunatangaza kwa mujibu wa utaratibu wetu,” alisema mwenyekiti huyo.

Alisema siku ya kwanza walipokea majimbo matatu na kuyatangaza na kwamba haikuwa rahisi kusubiri majimbo yote ndipo matokeo yatangazwe. “Tuliahidi kukamilisha kazi hii kwa wakati kwa kutangaza kwa kadri tunavyopokea, tukitangaza na ikaonekana mgombea fulani anaongoza ndivyo tunavyoyapokea na hatuwezi kusubiri yote ndiyo tutangaze,” alisema.

Aidha, alisema kauli ya kutaka busara itumike ni wazi kuwa hadi sasa NEC inatumia busara na ndiyo maana matokeo yanatangazwa na wanajitahidi kutimiza ahadi ya kuhakikisha mshindi anafahamika mapema.

Juzi, Lowassa anayeachwa mbali na Dk Magufuli, alidai NEC inaanza kutangaza maeneo iliyoshinda CCM ili kuaminisha umma kuwa chama hicho kimeshinda na kuwataka kutumia busara na uungwana.

Jimbo la Chalinze Magufuli 52,212, Lowassa 21,380 na Mghwira 450 Jimbo la Chonga Magufuli 1,740, Lowassa kura 3,860 65.85 na Mghwira 22. Jimbo la Chumbuni Magufuli kura 5,096, Lowassa kura 4,450 na Mghwira kura 31 Jimbo la Ileje Magufuli kura 26,368, Lowassa 15,651 na Mghwira 501.

Jimbo la Kijini Magufuli kura 2,703, Lowassa kura 3,351 na Mghwira kura 144. Jimbo la Kilindi Magufuli kura 33,941, Lowassa kura 12,123, Mghwira kura 324. Korogwe Mjini Magufuli kura 17,168, Lowassa kura 9,034 34.18 na Mghwira kura 151 Jimbo la Koani Magufuli kura 6,245, Lowassa kura 2,684 na Mghwira kura 14 Jimbo la Lupembe Magufuli kura 23,061, Lowassa kura 7,466, Mghwira kura 259.

Jimbo la Madaba Magufuli kura 13,949, Lowassa kura 4,735 na Mghwira kura 134. Jimbo la Masasi Mjini Magufuli kura 24,637, Lowassa kura 16,778 na Mghwira kura 266 Jimbo la Mbeya Vijijini Magufuli kura 62, 662, Lowassa kura 47,038 na Mghwira kura 672.

Jimbo la Mkwajuni Magufuli kura 4,686, Lowassa kura 3,314 na Mghwira kura 20. Jimbo la Momba Magufuli kura 28,978, Lowassa kura 24, 418 na Mghwira kura 406. Jimbo Monduli Magufuli kura 11,355, Lowassa kura 49,675 na Mghwira kura 107. Jimbo la Mpendae Magufulli kura 4,192, Lowassa kura 4,048 na Mghwira kura 14. Jimbo la Mwanga Magufuli kura 25, 738, Lowassa kura 15,148 na Mghwira kura 150.

Jimbo la Namtumbo, Magufuli kura 44,061, Lowassa kura 23,039 na Mghwira kura 566 Jimbo la Newala Mjini Magufuli kura 21,269, Lowassa kura 16,980 na Mghwira kura 202 Jimbo la Newala Vijijini Magufuli kura 29,799, Lowassa kura 13,388 na Mghwira kura 412. Jimbo la Muhambwe Mghwira kura 1,302, Magufuli kura 37,746 na Lowassa kura 22,804. Jimbo la Jang’ombe Mghwira kura 20, Magufuli kura 6,577 na Lowassa kura 2,839.

Jimbo la Malindi Mghwira kura 20, Magufuli kura 2,581 na Lowassa kura 5,622. Jimbo la Tabora Kaskazini Mghwira kura 508, Magufuli kura 38,050 na Lowassa kura 12,410. Jimbo la Unguja Kaskazini Mghwira kura 5, Magufuli kura 5,592 na Lowassa kura 1,019. Jimbo la Ole Mghwira kura 10, Magufuli kura 618, na Lowassa kura 5,251. Jimbo la Ziwani Mghwira kura 17, Magufuli kura 592, na Lowassa kura 6,067.

Jimbo la Wawi Mghwira kura 19, Magufuli kura 1,748, na Lowassa kura 5,216. Jimbo la Ulanga Mghwira kura 222, Magufuli kura 32,297 na Lowassa kura 20,489. Jimbo la Igalula Mghwira kura 342, Magufuli kura 28,747 na Lowassa kura 8,593 Jimbo la Tumbatu Mghwira kura 21, Magufuli kura 5,720, na Lowassa kura 3,967. Jimbo la Tandahimba, Mghwira kura 803, Magufuli kura 49,098, na Lowassa kura 46,288.

Jimbo la Solwa Mghwira 645, Magufuli 66,096, na Lowassa kura 23,510. Jimbo la Siha Mghwira kura 155, Magufuli kura 18,252 na Lowassa 22,572. Jimbo la Ruangwa Mghwira kura 319, Magufuli kura 34,516, na Lowassa kura 26,827. Jimbo la Magomeni Mghwira 10, Magufuli 5,716 na Lowassa 3,711. Jimbo la Werezo Mghwira 10, Magufuli 2,615 na Lowassa 2,582. Jimbo la Mkuranga Mghwira 899, Magufuli 45,710 na Lowassa 36,478.

Jimbo la Mafia Mghwira 146, Magufuli 11,155 na Lowassa 9,363. Jimbo la Nachingwea Mghwira 461, Magufuli 46,485 na Lowassa 30,252. Jimbo la Mwanakwerekwe Mghwira kura 12, Magufuli 4,206 na Lowassa 4,606. Jimbo la Kibaha Vijijini Mghwira kura 121, Magufuli kura 20,505 na Lowassa kura 11,344. Jimbo la Arusha Mjini Mghwira kura 464, Magufuli kura 65,107 na Lowassa kura 150,786.

Jimbo la Biharamulo Mghwira kura 605, Magufuli kura 44,943 na Lowassa kura 28,576. Jimbo la Tunguu Mghwira kura 18, Magufuli kura 8,519 na Lowassa kura 2,923. Jimbo la Mtama Mghwira kura 458, Magufuli kura 29.625 na Lowassa kura 20,841. Jimbo la Chwaka Mghwira kura 28, Magufuli kura 6,537 na Lowassa kura 1,864. Jimbo la Nungwi Mghwira kura 47, Magufuli kura 4,135, na Lowassa kura 4,853.

Jimbo la Amani Mghwira kura 18, Magufuli kura 4,322 na Lowassa kura 3,157. Jimbo la Nkenge Mghwira kura 307, Magufuli kura 42,568 na Lowassa kura 25,840. Jimbo la Nkasi Kusini Mghwira kura 246, Magufuli kura 21,572 na Lowassa kura 13,550. Jimbo la Chake Chake Mghwira kura 15, Magufuli kura 1,253 na Lowassa kura 5,209 Jimbo la Nkasi Kaskazini Mghwira kura 216, Magufuli kura 25,837 na Lowassa kura 19,891 Jimbo la Uzini Mghwira kura 30, Magufuli kura 10,879 na Lowassa kura 1,625.

Jimbo la Ugwini Mghwira kura 11, Magufuli kura 2,303 na Lowassa kura 2,822. Jimbo la Mwere Mghwira kura 19, Magufuli kura 6,430 na Lowassa kura 5,865. Jimbo la Mchinga Mghwira kura 203, Magufuli kura 13,948 na Lowassa kura 12,936. Jimbo la Mpanda Mghwira kura 699, Magufuli 37,321 na Lowassa kura 12,791. Jimbo la Kikwajuni Mghwira kura 13, Magufuli kura 6,317 na Lowassa kura 3,669.

Jimbo la Vuoni Mghwira kura 3, Magufuli kura 956 na Lowassa kura 420 Jimbo la Shaurimoyo Mghwira kura 32, Magufuli 5,849, na Lowassa kura 3,731 Katika majimbo ambayo matokeo yake yametangazwa juzi usiku ni: Jimbo la Kojani Mghwira kura 27, Magufuli kura 1,561 na Lowassa kura 9,982 Jimbo la Wete Mghwira kura 18, Magufuli 958, na Lowassa 5,119. Jimbo la Gando Mghwira kura 11, Magufuli kura 881, Lowassa kura 5,903.

Jimbo la Mtambwe Mghwira kura 9, Magufuli kura 428 na Lowassa kura 6,937. Jimbo la Mgogoni Mghwira kura 12, Magufuli kura 710, Lowassa kura 6,506. 


Jimbo la Kisarawe, Mghwira kura 235, Magufuli kura 24,086 na Lowassa kura 13,093. Jimbo la Mbinga Mghwira kura 329, Magufuli kura 29,295, na Lowassa kura 11,695. Jimbo la Nanyamba Mghwira kura 361, Magufuli kura 24,904, Lowassa kura 16,992.

Jimbo la Moshi Mjini Mghwira kura 149, Magufuli kura 28,909, na Lowassa kura 49,379. Jimbo la Mkinga Mghwira 228, Magufuli 23,798, Lowassa 15,142 Jimbo la Peramiho Mghwira 359, Magufuli 32,505, na Lowassa 11,291.HABARILEO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: