
Mgombea urais kupitia Ukawa Edward Lowassa leo ameshindwa kuhutubia mikutano miwili ya kampeni katika jimbo la Kilosa na Morogoro mjini kutokana na kubanwa na ratiba ya mikutano ya kampeni mkoani Morogoro.
Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara ulioandaliwa kwa ajili mgombea huyo wa nafasi ya urais, Mgombea ubunge wa jimbo la Morogoro Mjini Marcus Albanie aliwaelewa wanachama na wafuasi wa Ukawa katika uwanja wa Kiwanja cha Ndege kuwa Lowassa hawezi kufika katika viwanja hivyo kutokana na kubanwa na ratiba ngumu ya kampeni.
Albanie alisema kuwa Lowassa alitakiwa kuhutubia wananchi eneo hilo wakati akitokea Ifakara, Ruaha, Mikumi lakini ameshindwa na kuelekea Kibaha moja kwa moja.
Lowassa leo ameshindwa kuhutubia katika mikutano ya hadhara katika majimbo ya Mikumi, Kilosa na Morogoro.Chanzo.MTANDA BLOG

0 comments:
Post a Comment