
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amepata ajali mbaya akiwa njiani kuelekea Lindi akitokea jijini Dar es Salaam.
Nape amenusurika kifo katika ajali hiyo iliyotokea leo asubuhi katika eneo la Njia Nne Kilwa akiwa anatoka Dar kuelekea jimboni kwake.
Ajali hiyo ilitokea baada ya tairi la mbele la gari aliyokuwa akiendesha aina ya Toyota Land Cruiser kupasuka na kupinduka mara kadhaa.
"Namshukuru Mungu nimetoka salama na nawaomba wananchi wasiwe na hofu japo ajali ilikuwa mbaya maana gari lilipinduka mara kadhaa, nimepata majeraha madogomadogo na michubuko ila ni mzima".alisema NapeGari limeharibika vibaya ila ninachoshukuru nilikuwa nimefunga mkanda na 'air bag' nazo zimenisaidia."
Kabla ya ajali hiyo, Nape alikuwa jijini Dar es Salaam ambapo aliungana na mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Pombe Magufuli aliyekuwa na mikutano kadhaa ya kampeni katika jiji la Dar na baada ya shughuli hiyo alikuwa akirejea Lindi kuendelea na kampeni kwenye jimbo lake la Mtama.

0 comments:
Post a Comment