Kujiepusha na vikundi vyenye muonekano wa kuzalisha vurugu.
Picha hizi zinatoka katika maktaba ya MTANDA BLOG na zilikuwa zikihusisha tukio la mmoja wa vijana kumzalilisha askari wa kike wa kikosi cha jeshi la zima moto na Uokoaji eneo la fire Manispaa ya Morogoro tarehe 10 juni 2015 baada ya kuanzisha vurugu kwa kufunga barabara ya mtaa wa Mindu na kusababisha kutotumika kwa masaa kadhaa.
Oktoba
25 mwaka 2015 ni siku ya kuweka historia kwa Tanzania ambapo wananchi
wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea hasa wenye sifa watapiga kura
ya kumchagua kiongozi katika ngazi ya udiwani, ubunge na urais wa
kuongoza nchi baada ya rais aliyepo madarakani kumaliza muda wake
kulingana na matakwa ya katiba.
Jumapili ya Oktoba 25
ni siku ya kila mtanzania kuona siku hiyo ni muhimu kwake na yenye
furaha lakini siku hiyo inaweza kugeuka chungu endapo mtu atajiingiza
katika vurugu za namna yoyote na vyombo vya dola havitasita kuchukulia
hatua za kinidhamu.

Vurugu
hizo zinaweza kuzalishwa kwa mhusika endapo tu ataweza kutumia vilezi
kama pombe, sigara haramu (bangi) ambapo vitu hivyo huchangia
kumuondolea mtu akili zake za kufikili na kumpelekea kujiingiza katika
mambo yanayopingana na sheria za nchi.
Hapa kuna
matukio mbalimbali yanayoonyesha vijana waliovunja sheria za nchi lakini
askari wenye thamana ya kutuliza ghasia wanaonekana wakiwadhibiti
vijana hao.
Tukio hili ni tukio linalooonyesha vijana
na askari wanavyoweza kutekeleza majukumu yao lakini askari hao wamekuwa
na kawaida ya kuangalia nani amekuwa chanzo cha vurugu.
Hapo katika
picha ya pili hadi ya nne anaonekana kijana ambaye alikuwa kinara wa vurugu hizo kabla
na baada ya kumkamata na kumtia nguvuni.
Akili za kuambiwa changanya na zako, MTANDA BLOG inawatakiwa Tanzania wote siku ya jumapili Oktoba 25 tupige kura kwa amani na tusubirie matokea kwa njia iliyo ya utulivu ili kuendeleza amani iliyopo na siku hiyo isiwe siku ya kuanzisha vurugu, Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.AMINA.
CHINI KUNA MUENDELEZO WA MATUKIO HAYO.













0 comments:
Post a Comment