BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

VYAMA VYA SIASA VIWEKE WAKALA WAAMINIFU NA WAADILIFU ILI KUEPUSHA VURUGU.

Baadhi ya sehemu ya vijana zaidi ya 120 wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea wakati wa mdahalo wa utunzaji na kulinda amani katika uchaguzi kuu Oktoba 25 mwaka huu uliofanyika kwenye ukumbi wa Amani Center Kata ya Chamwino Manispaa ya Morogoro jana.PICHA/MTANDA BLOG

Juma Mtanda, Morogoro.

Morogoro.Vyama vya siasa vyenye wagombea katika ngazi ya uraisi,ubunge na udiwani vimeshauriwa kuwateua wakala waaminifu na waadilifu watakaoweza kusimamia kwa amani wakati wa upigaji na usimamiaji kura ili kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi.


Aidha ushauri huo umembatana na kuwataka wananchi kufuata sheria zilizopo na kukubaliana matokeo yatakayotangazwa kwa ngazi zote.


Akizungumza na vijana zaidi ya 120 katika mdahalo wa utunzaji wa kulinda amani, Afisa Mtendaji wa Kata ya Chamwino Manispaa ya Morogoro, Lawrance Masanja alieleza kuwa amani ya Tanzania mwaka huu ipo mikononi mwa mawakala endapo watatunza uaminifu na uadilifu wa kusimamia vyema zoezi la kuhesabu kura za wagombea na kukubali matokeo.


Masanja alieleza kuwa moja ya kazi kubwa ya mawakala wa mgombea ndani ya vyama vya siasa ni kusimamia zoezi zima la upigaji kura, kuhesabu kura na utangazaji wa matokeo ambao mgombea husika hupewa taarifa na wakala wake kinyume na hapo amani inaweza kutoweka.


“Uchaguzi una sehemu kuu tatu ambazo ni kujiandikisha katika daftari la mpigakura,wagombea kufanya kampeni na upigaji kura kumchagua mgombea katika ngazi za udiwani,ubunge na urais na katika upigaji wa kura kinachofuata ni kuhesabu kura,”alisema Masanja.


Aliongeza Masanja kwa kusema kuwa vyama vyote vinavyorishiki uchaguzi mkuu wanalazimika kuteua mawakala waaminifu lakini wawe na sifa ya uadilifu ili matokeo yatakapotangazwa baada ya zoezi la mwisho la uhesabuji kura wanatakiwa kuwa wakweli kwa kuwaeleza wagombea matokeo halisi yaliyojitokeza.


Aliwataka mawakala wasiwe chanzo cha vurugu na kupelekea amani kutokweka katika vituo vya kupigia kura, hivyo umakini wao utaepusha jazba kutoka kwa vijana ambao wengi wao wamekuwa na mihemuko ambapo baadhi ya matukio ya uvunjifu wa amani yamejitokea katika kipindi cha kampeni na kupelekea watu kupoteza maisha vilivyotokana na vurugu za kisiasa.


Mkurugenzi wa Mipango na Masoko Shirika la Morogoro Youth Development Initiative (Moyodei),Gasto Mgomoko alisema kuwa lengo la mdahalo huo umelenga kuwapatia elimu vijana namna ya utunzaji na ulindaji amani mara baada ya upigajikura katika uchaguzi mkuu kwani vijana wamekuwa wakitumika vibaya na baadhi ya wanasiasa.


Mgomoko alisema kuwa vijana wamekuwa wakitumika katika matukio ya vurugu na wamekuwa mstari wa mbele baada ya kuhamasishwa na viongozi katika kufanikisha azma yao ya kisiasa jambo ambalo limekuwa hatari kwa hasa vyombo vya dola vinapokabiliana nao kutuliza.


“Shirika letu limekuwa likitoa elimu katika jamii hasa vijana katika njanya za siasa, kilimo, ujasiliamali na leo (jana) tumekusanya vijana zaidi ya 120 ili kuwapa mambo muhimu ya kuepuka siku ya upigaji kura na tumawaelisha namna ya kutunza amani.”alisema Mgomoko.


Vijana wasitumike kuanzisha vurugu na kuepuka mihemko na endapo watashindwa kuhimili mambo hayo watajikuta wakitumbukia katika vyombo vya ulinzi kwa kuanzisha vurugu mara baada ya zoezi la upigaji kura na kutangazwa kwa matokeo.


“Tanzania yenye furaha na amani itadumishwa na vijana ambao wana umri mrefu wa kuishi kuliko rika nyingine na kama vijana wasipokjitambua na kutunza amani waatajikuta wakiishi katika maisha yasiyotarajiwa kwani amani ni kila kiti”.alisema Mgomoko.


Mariamu Lupinda (36) mkazi wa Kiwanja cha Ndege mmoja wa vijana walioshiriki mdahalo juo alisema kuwa baada ya watu kupiga kura jambo la msingi ni kurudi nyumbani hata hao baadhi ya wana siasa kwani hata kama wataendelea kukaa mita 200 haoni kama kuna mantiki.


Lupinda alisema haoni mantiki ya kukaa mitaa 200 kutoka eneo la kituo cha kupigia kura kilipo na umabli huo macho ya mwanadamu hana uwezo wa kuona tukio la kuhesabuji kura ndani ya chumba na pengine muda huo ungefaa kufanya shughuli .


“Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) na mawakala wataosimamia zoezi zima la upigaji kura ni vyema tukawa na imani na kiongozi wa kisiasa anaposema tulinde kura kwa kukaa mitaa 200 huko ni kujidanganya,”alisema Lupinda.CHANZO/MTANDA BLOG
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: