Mbunge wa Morogoro Mjini (CCM), Abdulazizi Abood Na Lilian Lucas.
Mbunge wa Morogoro Mjini (CCM), Abdulazizi Abood amewatoa hofu ya kubomolewa nyumba zao wakazi wa Mtaa wa CCT, Manispaa ya Morogoro baada ya nyumba 15 za mtaa huo kubomelewa kwa makosa.
Nyumba hizo zilibomolewa Desemba 3, baada ya kudaiwa kujengwa ndani ya hifadhi ya msitu wa kuni uliopo mpakani mwa Wilaya ya Mvomero na Manispaa ya Morogoro.
Alisema baada ya uongozi wa manispaa kuzungumza na idara ya misitu, ilibainika kuwa eneo hilo lilitolewa kihalali kwa wakazi hao na Mkoa wa Morogoro kipindi cha miaka ya 80.
Mmoja wa wakazi wa mtaa huo, Nashir Kamgisha pamoja na kumpongeza mbunge huyo kwa juhudi zake alizozionyesha, alimuomba kuingilia kati suala la upimaji wa viwanja alilodai kuwa gharama zake ni kubwa.

0 comments:
Post a Comment