Juma Mtanda, Morogoro.
Klabu ya Burkina FC imemtupia lawama mwamuzi wa kati, Amour Juma kutoka Pwani kufuatia kuambulia sare ya bao 2-2 wakimtuhumu kuipendelea Polisi Moro SC wakati wa mchezo wao wa ligi daraja la kwanza Tanzania bara uliofanyikakwenye uwanja wa jamhuri jana (juzi) mkoani Morogoro.
Katika mchezo huo, Burkina FC walipoteza nafasi nyingi za wazi za kufunga mabao kutokana na safu yao ya ushambuliaji kutokuwa makini hasa wanasogelea eneo la hatari hali iliyowalazimu kuambulia sare hiyo na kuendelea kuruza mkia katika msimamo wa ligi hiyo kundi A.
Polisi Moro ndio walianza kupachika bao la kuongoza dakika ya 18 kupitia kwa, Ally Telu akitumia vyema makossa ya walinzi wa Burkina walioshindwa kuondoa hatari langoni mwao baada ya Nahoda Bakari kuchongwa kona iliyomkuta mfungaji kabla ya Mshambuliaji, Victor Mswaki kuisawazishia Burkina bao dakika ya 41.
Mswaki alifunga bao hilo kutokana na uzembe wa walinzi wa Polisi Moro katika eneo la hatari kwa kukosa mawasiliano kati ya kipa na walinzi hao lakini dakika ya 56, mshambuliaji mkongwe Ulimboka Mwakingwe aliandikia Burkina bao la pili makosa ya kujirudia huku, Nicolaus Kabipe akisawazisha kwa kufunga bao la pili kwa Polisi Moro SC katika mchezo huo.
Kocha wa klabu ya Burkina FC, Allan Yahaya alimwandama mwamuzi wa mchezo huo kwa kushindwa kufuata sharia 17 za mchezo huo baada ya kudai kuinyima adhabu ya penalti mbili timu yake baada ya wachezaji wa Polisi Moro kufanya madhambi eneo la hatari.
“Nimekuwa nikilalamikia waamuzi siku zote hasa wale wasilofuata sharia 17 za mchezo wa soka na sina ugomvi na waamuzi wanaofuata sharia 17 za soka lakini mwamuzi wa leo (juzi) kama angekuwa makini ilimpasa atoe adhabu ya penalti mbili kutokana na wachezaji wa Polisi Moro kufanya madhambi eneo la hatari.”alisema Yahaya.
Kwa upande wa kocha mkuu mpya wa klabu ya maafande hao, Joseph Lazaro alieleza kuwa mchezo huo ulitawaliwa na presha kutoka kwa mashabiki hali iliyosababisha na wachezaji nao kukumbwa na presha hiyo.
Kutokana na mwenendo mmbaya wa klabu hiyo ya Burkina FC imeendelea kuburuza mkia katika msimamo wa ligi katika kundi A ikiwa imekusanya pointi tatu huku Polisi Moro SC ikiwa tayari imeweka kibindoni pointi 11 mbele ya vinara wa kundi hilo Ruvu Shooting inayoongoza kundi hilo.CHANZO:MTANDA BLOG

0 comments:
Post a Comment