BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAJAMBAZI WAWAPONZA WAFANYABIASHARA WA MADAWA YA KULEVYA JIJINI DAR ES SALAAM.

Picha ya maktaba yakionekana magunia yenye bangi.

Dar es Salaam. Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam inawashikilia watu 71 kwa tuhuma mbalimbali ikiwamo ujambazi wa kutumia silaha na pikipiki aina ya Boxer.

Kamishna wa Polisi wa Kanda hiyo, Suleiman Kova amewaambia wanahabari leo kuwa kati ya watuhumiwa 71 wanaoshikiliwa, wanne walikutwa na bunduki tatu aina ya Shotgun na Pump action pamoja na bastola moja.

Amesema silaha hizo zilitumika katika matukio kadhaa ya kihalifu na likiwamo la tukio la uporaji lililotokea Selender Bridge, Manispaa ya Ilala.

“Kama mnavyojua kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kumekuwa na matukio kadhaa ya majaribio ya uvunjifu wa amani na uporaji. Hata hivyo polisi imejipanga ipasavyo kupambana na hali hii.

“Watuhumiwa hawa 71, wamekamatwa katika kipindi cha wiki moja kufuatia operesheni tunayoendelea kuifanya kipindi hiki cha mwisho wa mwaka,” amesema Kamishna Kova.

Amefafanua kuwa watuhumiwa 67 walikamatwa kwa tuhuma za kukutwa na dawa zinazodhaniwa ni za kulevya aina ya bangi magunia 100 na kete 48 za heroin na Cocane.

Hata hivyo, magunia hayo yalikamtwa maeneo ya Kimara, yakiwa katika gari ndogo aina ya Carina.

Ameongeza kuwa, uchunguzi wa awali umebaini kuwa dawa hizo zilikuwa zikitokea mkoani Morogoro na zilifika Dar es Salaam kwa ajili ya kuuzwa na kusambazwa maeneo mengine.

Katika hatua nyingine, Kamishna Kova amesema polisi ikishirikiana na kampuni binafsi za ulinzi Dar es Salaam, limepanga kuimarisha ulinzi kuanzia katika nyumba za ibada siku ya mkesha na sikukuu ya mwaka mpya.

Wakati huohuo, Kamishana Kova amesema Jeshi la Polisi limeanza na msako wa kuwatafuta watu waliohusika na vurugu kati ya maofisa wa ardhi na wakazi wa eneo la Jangwani. 


Amesema kufuatia kadhia hiyo walioipata maofisa hao , Kamishana Kova amesema ameamua kuongeza askari zaidi katika eneo hilo ili kuwarahisishia maofisa ardhi kufanya kazi yao kwa ufanisi na bila bughuza.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: