BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SERIKALI YAJIANDAA KUFUMUA MTANDAO WA WAUZA MADAWA YA KULEVYA, MITEGO YATENGWA KILA KONA YA KUWANASA WAFANYABIASHARA.

Picha ya maktaba ikionyesha madawa ya kulevya baada ya kukamatwa Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Serikali imejipanga kukabiliana na biashara ya dawa za kulevya nchini kwa kuandaa mikakati itakayohakikisha mtandao wa wanaojihusisha nayo unavunjwa.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga alitangaza mpango huo jana kwa lengo kuondoa madhara yatokanayo na matumizi yake kwenye jamii hasa vijana.

“Jeshi limejipanga kukabiliana na biashara hii. Tumeandaa mfumo ambao utazuia dawa zote zinazoingia nchini na kuwakamata wote walioziingiza pindi tu watakapojaribu kuzisambaza, “ alisema na kusisitiza kuwa:

“Huu ni mpango endelevu wa kuhakikisha matumizi ya dawa hizi yanakomeshwa kwa kuzuia upatikanaji wake.”

Katika utekelezaji wa mapambano hayo, waziri alionya kuwa yeyote atakayebainika atakamatwa bila kujali wadhifa wake serikalini au kwenye jamii anayoihudumia na kufikishwa mahakamani. Hata hivyo, Kitwanga alikanusha kupokea orodha ya wauza dawa hizo kama baadhi ya wadau wanavyodai.

Alisema utekelezaji wa jambo hilo utaanzia kwenye Bandari ya Dar es Salaam ili kudhibiti ubadhirifu na rushwa, vitendo ambavyo vimeipaka tope sekta hiyo.

Kwa upande mwingine, Kitwanga alisema Kikosi cha Usalama Barabarani cha Jeshi la Polisi nchini kimejidhatiti kupunguza msongamano wa magari ili kurahisisha mzunguko wa kutoka sehemu moja kwenda nyingine hasa maeneo ya katikati ya miji mikubwa nchini.

“Ili kufanikisha hayo yote upo mpango wa kuboresha makazi ya askari. Tunaupungufu wa nyumba 35,000 ili kuwatoshereza watumishi wote wa jeshi hili,” alisema.

Takwimu zinaonyesha kuwa kati ya askari 45,000 wa Jeshi la Polisi 10,000 ndiyo wanaoishi kwenye nyumba za Serikali na kwamba zinahitaji hatua za haraka kukabiliana na janga hilo.

Waziri Kitwanga alitoa wito kwa askari kuacha kuwabambikizia kesi raia na kuagiza yeyote anayeshikiliwa kushtakiwa kwa makosa yanayomkabili na kuchukuliwa hatua. Mkuu wa Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu aliitaka jamii kuepuka uzushi wa mambo isiyoi na na uhakika nayo akisema ni kinyume cha sheria.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: