Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 131.4 kwa ajili ya kugharamia uendeshaji wa shule za msingi na sekondari ili kuziba pengo la michango iliyokuwa ikichangishwa mashuleni.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI ,Utumishi na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana.
Mheshimiwa Simbachawene alisema serikali imechukua jukumu la kulipia michango yote iliyokuwa ikitolewa na wazazi na walezi wa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ili kuziba pengo la michango hiyo.
Alisema dhana ya elimu bila malipo inazingatia uendeshaji wa shule bila ada wala michango yeyote ya lazima kutoka kwa wazazi au walezi wa wanafunzi.
Waziri Simbachawene alisema fedha zilizotolewa na serikali kwa ajili ya kugharimia elimu zitapelekwa moja kwa moja shuleni kutoka HAZINA kwa wastani wa shilingi bilioni 18.777 kwa ajili ya ruzuku za shule kila mwezi.
Alifafanua kuwa ruzuku hizo za gharama za uendeshaji wa shule ni shilingi 10,000 kwa wanafunzi wa shule za msingi na shilingi 25,000 kwa wanafunzi wa sekondari kwa mwaka.
Alisema wanafunzi wa sekondari wanaokaa shule za bweni na msingi watapata shilingi 1500 kwa siku ikiwa ni pamoja na fidia ya sh 20,000 kwa wanafunzi wa kutwa na sh. 70,000 kwa wanafunzi wa bweni kidato cha kwanza hadi cha nne.
Mheshimiwa Simbachawene alisema gharama za mitihani ya kidato cha nne zitalipwa na serikali moja kwa moja Baraza la Mitihani hivyo wazazi na walezi hatawatawajibika kugharamia tena.
Naomba ieleweke kwamba dhana ya elimu bila malipo haiondoi dhamira ya uzalendo kwa jamii kushiriki kwa hiari kuchangia michango katika kuleta maendeleo ya elimu hapa nchini “alisema Mhe. Waziri
Mhe. Simbachawene alisema wazazi na walezi watawajibaka kununua sare za shule ,michezo, magodoro na mashuka ,vifaa vya usafi binafsi,vifaa vya kujifunzia vikiwemo madaftari,kalamu na chakula kwa wanafunzi wa kutwa.
Mahitaji mengine ambayo wazazi wanatakiwa kugharamikia ni matibabu kwa watoto wao,nauli za kwenda na kurudi shule kwa wanafunzi wa kutwa na kwa wanafunzi wa bweni wakati wa likizo.
Wakati huo katika taarifa iliyotolewa kwa niaba ya Waziri huyo na Mkuu wa Kitengo cha MawasilianoSerikalini wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bibi Rebecca Kwandu, ilisema kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. George Simbachawene amemwagiza mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma kuwasimamisha kazi mara moja Kaimu Afisa Biashara Bw.Elias Kamara na Afisa Biashara Bibi Donatila Vedastokutokana na makosa waliyoyafanya katika utendaji wao wa kazi.
Alitaja sababu za kusimasishwa kwao kuwa ni kutokana na kuisababishia hasara manispaa hiyo ya jumla ya shilingi milioni 75 kutokana na urasimu wa utoaji leseni za biashara.
Alisema katika uchunguzi uliofanywa katika halmashauri hiyo ya Manispaa ya Dodoma imegundulika kuwa kulikuwa na maombi 750 ya leseni ambayo yalikuwa hayajashughulikiwa bila sababu za msingi.
Alisema mhe. Simbachawene ameagiza watumishi hao wachukuliwe hatua za kinidhamu wakati ikiwepo kusimamishwa kazi wakati uchunguzi dhidi yao ukifanyika.chanzo:Mzee wa Matukio.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / SERIKALI YAKATA MZIZI WA FITINA KWA KUTENGA FEDHA SH 131.4 BIL KWA AJILI YA UENDESHAJI ELIMU YA MSINGI NA SEKONDARI
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment