BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WATU WANAODHURU MIFUGO KWA MAKOSA YALIYOFANYWA NA BINADAMU YAMKERA WAZIRI MWIGULU NCHEMBA.

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba      

Dar es Salaam. Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi imeonya dhidi ya vitendo vya kuhukumu wanyama kwa makosa yanayofanywa na binadamu, ikisema ni kinyume cha sheria na ni ukatili.

Mapema mwezi huu kulitokea mapigano baina ya wakulima na wafugaji kwenye Kijiji cha Dihinda, Mvomero ambayo yalidumu kwa takriban siku tatu na kusababisha mauaji ya mtu mmoja, ngo’mbe 79, huku wengine 72 wakijeruhiwa kwa mapanga.

Siku moja baada ya tukio hilo waziri wa wizara hiyo, Mwigulu Nchemba alitembelea eneo hilo na kuagiza wahusika wakamatwe na viongozi wa vijiji watenge maeneo ya wakulima na wafugaji ili kuepuka migogoro isiyokoma.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, mkurugenzi huduma za mifugo, Dk Abdul Hayghaimo alisema kwa mujibu wa Sheria ya Ustawi wa Wanyama ya Mwaka 2008, Sura ya 154 kifungu cha 4, wanyama wana haki ya kupewa chakula, maji, mahali pazuri pa kupumzika na kulindwa dhidi ya maumivu yoyote yanayoweza kuwasababishia kifo.

“Wizara inakemea vikali tabia ya kuadhibu wanyama kwenye maeneo yenye migogoro kati ya wakulima na wafugaji na inawataka wananchi wenye tabia hiyo kuacha mara moja, kwa kuwa makosa hayo hufanywa na binadamu kwa kuwaongoza na siyo wanyama wenyewe,” alisema Hayghaimo.

“Pia kifungu cha 49 na 58 cha sheria hiyo kinaainisha taratibu za kufuatwa pale mnyama anapokutwa kwenye eneo lisiloruhusiwa, hivyo vitendo vilivyofanyika dhidi ya wanyama kwenye Kijiji cha Dihimba ni kosa kwa mujibu wa sheria.”

Ofisa habari wa wizara hiyo, Judith Mhina alisema kupitia tamko lake, wizara imewatahadharisha wananchi wanaochukua sheria mikononi na kusababisha madhara yasiyokubalika kutokana na migongano ya wakulima na wafugaji.

Wizara iliitaka jamii kutafuta njia mbadala ya suluhisho la migogoro kupitia kamati zitakazosimamia matumizi endelevu ya ardhi, kwa mujibu wa waraka ulioandaliwa na wizara kwa kuzingatia taratibu kanuni na sheria husika.

Vilevile, alisema Serikali imepanga kuwachukulia hatua stahiki wale wote waliohusika katika mauaji ikiwa ni sehemu mojawapo ya utekelezaji wa sheria dhidi ya ukatili kwa wanyama. 


Migogoro ya wakulima na wafugaji imekuwa changamoto kubwa kwa Serikali na wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu, Rais John Magufuli alitoa ahadi ya kuikomesha tatizo hilo.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: