BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BAADA YA KUONEKANA KWA PICHA ZA VAZI LA KIJESHI KWA RAIS WA TANZANIA, JOHN MAGUFULI NA RAIS UHURU KENYETTA WA KENYA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII, USAHIHI WA VYEO NI NDIYO HUU.


1. Dkt. JPM si Rais wa kwanza ndani ya JMT kuvaa nguo/Gwanda za Jeshi. Mwl. Nyerere aliwahi kuwa akivaa huko nyuma na hata wakati wa Vita ya Uganda.


2. Magwanda ya Marehemu Baba wa Taifa hayakuwahi kuwa na cheo.


3. Aidha, Jeshi ni taasisi ambayo imejengwa kwenye mifumo, sheria, miongozo na taratibu imara ambazo hazipaswi kuingiliana na mifumo ya kisiasa. Izingatiwe kuwa Vyeo ni lazima vitokane na mafunzo na elimu na utumishi husika.


4. Rais wa awamu ya nne alikuwa ni mwanajeshi wa cheo cha Luteni Kanali. Hata kama angeamua siku moja kuvaa Gwanda wala asingeweza kuvaa kwa cheo chake bali angevaa plain kwa hadhi yake kama Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama.


5. Aidha uvaaji wa magwanda ya kijeshi kwa ngazi ya Rais si jambo la kisheria na hivyo lilazimishe ama kunyambulisha masharti ikitokea mkuu wa nchi anataka kuyatumia.


6. Jeshi letu halijawahi kubuni cheo cha Amiri Jeshi Mkuu kwa kuwa kimafunzo na kitaratibu cheo kikuu cha mwisho ndani ya Jeshi letu ni Generali.


7. Yawezekana Gwanda alilovaa uhuru Kenyetta wasio na uweledi wa Kijeshi wasijue tafsiri yake... kile ni cheo cha "Field Marshall " ambacho kwa taratibu za kijeshi hutunukiwa baada ya kuwa amepiganisha vita nyingi na kuwa bingwa wa ""Utaalam/Medani za kivita!! kwa taratibu za kijeshi vazi la Kenyetta ni "kituko"
8. 


Museven kumbukeni ni Mwanajeshi wa Cheo cha U-Jenerali...hivyo kwake kuvaa Gwanda kwa vyeo hivyo ni sahihi hakuna shida. Na hupigiwa saluti kwa nafasi yake kama Amiri Jeshi Mkuu na siyo vyeo alivyovaa.

9. Mwisho: Mfumo wa Jeshi haupigii saluti vyeo/gwanda bali "mtu/status" kwa cheo chake. 


Ndiyo maana mwanajeshi wa cheo fulani huendelea kupigiwa saluti hata pale ambapo hayuko kwenye uniform ya kijeshi yenye vyeo. 

Au fanya hivi "Mwanajeshi wa cheo cha Ujenerali avue Gwanda lake lenye cheo husika na atundike kwenye mti na yeye aende mti jirani akiwa hata kifua wazi akae. 

Atakapopita mwanajeshi wa cheo cha chini hatayafuata magwanda na kuyapigia Saluti bali atamfuata Askari wa Cheo cha Ujenerali na kumpigia saluti!!

Ni hayo tu machache baada ya kuongea kushauriana na wenzangu.
 SOMO: 
Watanzania tujifunze kuwa si wajuzi wa kila kitu na si kila lifanywalo na wengine wa nje ni sahihi....mengine huwa ni vituko kwa wenye weledi wa eneo husika!
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: