Maji ya mafuriko yakipita juu ya daraja la zamani la Mbulumi na kusababisha barabara kuu ya Turiani-Morogoro kushindwa kutumika kwa masaa 22. Picha na Juma Mtanda, Morogoro.
Juma Mtanda, Morogoro.Zaidi ya magari 75 pamoja na wasafiri wamekwama kwa masaa 22 baada ya maji ya mafuriko kupita juu ya daraja la zamani la mto Mbulumi kufuatia mvua kubwa kunyesha mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro huku ikisababisha mawasiliano ya barabara kuu kushindwa kupitika kati ya mji mdogo wa Turiani na Morogoro mjini.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii eneo la daraja la Mbulumi leo (jana), Diwani wa kata ya Mhonda wilaya ya Mvomero mkoa wa Morogoro, Abdallah Alifa alieleza kuwa mvua iliyonyesha juzi katika mikoa ya kanda ya kaskazini ndio iliyosababisha maji ya mafuriko kupita juu ya daraja la chini la mto Mbulumi.
Mafuriko hayo yalisitisha huduma za usafiri kwa muda baada ya na kushindwa kupitika kwa masaa 22 huku magari zaidi ya 75 yakikwama kuendelea na safari zake.
Alifa alisema kuwa maji hayo yalikuwa na kasi na yalianza kukata mawasiliano ya barabara majira ya saa 7 mchana jana (juzi) na leo (jana) hadi saa 4 asubuhi na maji kupungua kasi ya kupita juu ya daraja na magari kuanza kupita baada ya kazi ya kuondoa magogo yaliyokwama juu ya daraja hilo.
“Mvua iliyonyesha juzi katika mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro imesababisha mafuriko na kuleta athari hasa kwa wakazi wa mabondeni na kukata mawasiliano ya barabara ya Turiani na Morogoro mjini kwa masaa 22”.alisema Alifa.
Alifa alisema licha ya maji hayo kukatakaa mawasiliano, zaidi ya kaya 25 za eneo la Msufini kijiji cha Kichangani wakumbwa na maji ya mafuriko yam to Mbulumi na kuharibu mali ikiwemo mifugo, chakula na mazao kuharibika.
Kwa upande wa wakazi wa mtaa wa Msufini kijiji cha Kichangani imeleta maafa baada ya maji hayo kubomoa kingo za mto Mbulumi na maji hao kuharibu mali katika kaya zaidi ya 25 za wakazi hao.
moja wa waathirika wa mafuriko hayo mkazi wa eneo la Msufini, Fatuma Omari alisema kuwa mafuriko yalianza kuingia katika majira ya saa 9 alasiri na kuingia katika nyumba na kufanya uhalibifu wa mali mbalimbali.
Fatuma alisema kuwa baada ya kuingia kwa maji hayo kumetokea uhalibifu wa mali kwa kusomba mifugo (kuku) kuharibu chakula ndani ya nyumba na mashambani.
“Baada ya mafuriko kuvamia katika makazi yetu, watu wengi tumehifadhiwa kwa majirani lakini tunamshukuru mwenyezi mungu hakuna binadamu aliyepoteza maisha”alisema Fatuma.
Wakati maji yapita juu ya daraja la chini la Mbulumi, kundi la vijana 12 lilitumia fursa ya kuvusha magari madogo kuyapitisha katika daraja jipya ambalo ujenzi wake haujakamilika kwa kutoza kiasi cha 5,000 hadi sh500 na kukusanya kiasi cha 213,000 kutokana na kazi hiyo.
Kiongozi wa vijana hao, Eboso Abdallah (27) aliliambia gazeti hili kuwa baada ya maji kupita juu ya daraja la zamani, walivusha magari kwa kuweka mbao katika kingo ya daraja jipya na kuwatoza madereva kiasi cha sh5,000 kwa gari ndogo na sh1,000 pikipiki.
Abdallah alisema tangu kuanza kwa maji hao kupita juu ya daraja majira ya saa 7 mchana juzi walivusha jumla ya magari madogo 16, jana magari 10 na pikipiki zaidi ya 50 na kujikusanyia kiasi cha sh213,000.
“Maji ya safari hii yamekuwa na nguvu kwani yamekuwa yakisimba magogo makubwa na mengi yao yamekwama katika darja linalotumika sasa hivi lakini limetoa fursa ya ajira ya muda mfupi na tumepata sh213,000 ambazo tutagawana vijana 12”alisema Abdalla.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

0 comments:
Post a Comment