Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Leticia Nyerere aliyefariki dunia wiki iliyopita nchini Marekani umewasili leo jijini Dar es Salaam.
Marehemu Leticia alifariki dunia akiwa Maryland nchini Marekani alikokuwa akipatiwa matibabu.
Kabla ya mauti kumkuta, alijiunga na CCM mwaka jana baada ya kutofautiana na viongozi wa Chadema.
Leticia
Historia fupi ya marehemu Leticia
Alizaliwa mwaka 1959, Kwimba mkoani Mwanza na kusoma katika Shule ya Msingi Mnazi Mmoja kati ya mwaka 1966 hadi 1973.
Kati ya mwaka 1974-75, alisoma Shule ya Sekondari Jangwani kidato cha kwanza hadi cha nne na 1976-78 alisoma kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari ya Arusha Meru.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN.

0 comments:
Post a Comment