BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SERIKALI YAWATOA HOFU WATANZANIA KWA KUWAELEZA HAKUNA ATAYEKUFA KWA NJAA

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuna akiba ya kutosha ya chakula huku kazi ya kugawa, kupeleka maeneo yote yenye mahitaji inaendelea na hakuna Mtanzania atakayekufa kwa njaa.

Aidha, amesisitiza marufuku ya upikaji wa pombe kwa kutumia chakula cha njaa na kile cha bei nafuu ili kupunguza makali ya njaa.

Waziri Mkuu alisema hayo juzi wakati alipofanya ziara ya kutembelea kijiji cha Majereko wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma ambacho ni miongoni mwa vijiji vilivyoathirika na njaa na kuwalazimu wananchi kuishi kwa kula zambarau na baadhi ya wadudu.

Alisema kuanzia sasa ni marufuku kutumia chakula cha msaada kwa ajili ya kupikia pombe na kila mmoja awe askari wa mwenzake na watakaobainika kufanya hivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Alisema chakula kinachotolewa na serikali ni kwa ajili ya kukabiliana na njaa na siyo kutumika kwa matumizi mengine. Alisema sasa serikali inasambaza chakula hicho katika maeneo mbalimbali nchini ni muhimu kikatumika kama ilivyokusudiwa.

“Tuna kazi ya kugawa na kupeleka maeneo yenye mahitaji makubwa,” alisema.

Alisema hivi karibuni wilaya hiyo imepatiwa tani 1,620 za chakula na kitasambazwa maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo na serikali itapeleka chakula kingine cha bure tani 40 ili wananchi wagawiwe.

“Juzi tulipeleka tani 700 kwa wananchi walioathirika na mafuriko na tutafanya hivyo ili kunusuru maisha ya wananchi,” alisema na kuongeza kuwa ghala la hifadhi ya chakula la Dodoma lina tani 12,000.

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Farida Mgomi alisema wilaya hiyo ilikusudia kupata tani 68,000 katika msimu wa kilimo, lakini kutokana na mvua kuwa chache, zilipatikana tani 34,216 na hivyo kufanya kuwa na upungufu wa chakula.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: