Na Juma Mtanda, Kilombero.
Zoezi
la kusaka miili ya abiria katika ajali ya kupinduka kwa kivuko cha MV
II Kilombero limeonekana kukubikwa na changamoto mbalimbali ikiwemo
ugumu wa kuopoa kivuko kutokana na ongezeko kujaa na kasi ya maji katika mto Kilombero mkoani Morogoro.
Akizungumza
na wandishi wa habari eneo la kivuko cha mto Kilombero, Meneja wa
Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa) Mhandishi Margreth Mapela alisema
kuwa ugumu wa zoezi la kukiopoa kivuko cha MV11 Kilombero na kupata
maiti kutokana na ongezeko la kujaa na kasi ya maji katika mto huo.
Mapela
alisema kuwa baada ya kukumbwa na changamoto hizo, tayari gari la
kunyanyua vitu vizito (Clean ya Temesa) pamoja na lile la kampuni ya
ujenzi ya daraja la kudumu la mto huo vimefika eneo la tukio ili kuweza
kufanya kazi ya kuopoa kivuko hicho.
“Kuna
ugumu wa zoezi la kuopoa kivuko cha MV II Kilombero na kuangalia kama
kuna uwezekano wa kupata maiti kama watakuwa wamekwama katika
kivuko.”alisema Mapela.
Mapela
alisema kuwa tayari kikosi cha JWTZ kimewasiri jana (juzi) na kuanza
kutoa huduma za kuvusha watu na wengine wakiendelea na kazi ya kukiibua
kivuko kwa kushirikiana na kampuni ya M. Divers Ltd ya Dar es Salaam ambapo watalaamu wao wamefanikiwa kuokoa baiskeli mbili na zoezi hilo linaendelea.
Lengo
lao kuzamia wataalamu hao ni kuanza kuchunguza kisha kuweka maboya
ambayo yatafanikisha kukiibua kivuko hicho na hatua itayofuata ni
kukivuta na kukitoa nchikavu.
Wakati
watalaamu wa kampuni ya M. Divers Ltd wakishirikiana na Temesa, JWTZ
katika kukiibua kivuko cha mto Kilombero, watalaamu wengine wa kampuni
ya May-Marine Go Ltd wamekuwa na kazi ya kutafuta magari ili kuyaibua.
Mkurugenzi
wa M. Divers Ltd, Salvatory Murungi alisema kuwa uwepo wa eneo hilo
umetokana na kuongeza nguvu katika kazi za kuibua magari likiwemo la
benki ya CRDB inayodhaniwa ndani ya gari yake kuwa na mtu na magarin
mengine mawili.
Murungi
alisema kuwa kazi iliyopo mbele yao leo (jana) ni kuanza kazi ya
wazamiaji wake kuzamia majini kutafuta gari hazi chini ya maji na baada
ya kuonekana yatafungwa maboya ili yaweze kuibuka yenyewe na kufunga
kamba kuyatoa nchikavu.
Kutokana
na kivuko cha MV II Kilombero kupinduka januaria 25, kumejitokeza na
mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali katika baadhi ya wilaya ya Ulanga.
Akizungumza
na gazeti hili kwa njia ya simu, Diwani wa kata ya Isongo wilaya ya
Ulanga, Henry Barua alisema kuwa baadhi ya wafanyabiashara wametumia
mwanya wa kukosekana kwa huduma za kivuko hicho, kumekuwa na mfumuko wa
bei wa bidhaa muhimu.
Barua
alisema kuwa baadhi ya wafanyabiashara wilaya hiyo wametumia mwanya huo
kupandisha bei ya bidhaa muhimu kufuatia kivuko hicho kupinduka.

0 comments:
Post a Comment