BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KAMANDA SELEMAN KOVA AMHENYESHA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA JESHI LA POLISI BAADA YA KUSTAAFU UPOLISI.


Aliyekuwa Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam , Suleiman Kova akizungumza katika moja ya mikutano na waandishi wa habari.

Arusha. Mahakama ya Rufani imetupa rufaa ya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Godfrey Nzowa dhidi ya Kamishna mstaafu wa jeshi hilo, Suleiman Kova na wakala wa majengo Tanzania (TBA), wanaogombea nyumba ya Serikali kwa sababu iliwasilishwa nje ya muda.

Nzowa alikata rufaa kupinga hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, iliyotolewa na Jaji Fatuma Masengi mwaka 2013, ikimpa Kova haki ya kumiliki nyumba hiyo.

Wakati hukumu hiyo ikisomwa jana saa sita mchana, Kova hakuwapo mahakamani lakini Nzowa ambaye ni mkuu wa kikosi cha kuzuia dawa ya kulevya nchini, alikuwapo tangu saa tatu asubuhi.

Majaji watatu wa mahakama ya rufani, Mbarouk Salum, Bernard Luanda na Mussa Kipenka walisema kuwa wametupa rufani hiyo kutokana na kuwasilishwa nje ya muda wa kisheria wa siku 60.

Akisoma uamuzi wa majaji hao, Naibu Msajili wa mahakama wa rufani, Elizabeth Mkwizu alisema pamoja na kuondolewa kwa rufani hiyo, Nzowa anatakiwa kulipa gharama za kuisikiliza.

Alisema kwa kuwa suala la muda wa rufani ni la kisheria, kwa vyovyote vile haiwezekani kupokelewa nje ya wakati kwani kufanya hivyo ni sawa na kupokea waraka batili.

Mkwizu alisema majaji wamejiridhisha na pingamizi ambalo liliwasilishwa na mawakili wa TBA na mawakili wa Serikali, Harun Matagane na Sylivesta Mwakitalu.

Alisema ingawa Wakili wa Nzowa, Mpaya Kamara alieleza mahakama kuwa kosa la kucheleweshwa rufani halikuwa lao bali ni la maofisa wa mahakama, majaji wametoa uamuzi huo kwa kuzingatia uhalali wa rufani hiyo.

Hata hivyo, alisema wakata rufani bado wana nafasi ya kuiwasilisha upya kwa kufuata taratibu za mahakama.

Akizungumza baada ya uamuzi huo, wakili Neema Mtayangulwa anayemtetea Nzowa alisema watajadiliana hatua za kuchukua kwa kuwa uamuzi huo si mwisho wa kutafuta haki.

Katika kesi hiyo, Kova ambaye jana alikuwa anaagwa na jeshi la polisi baada ya kustaafu, alikuwa anatetewa na mawakili, Dilip Kesaria na Pascal Qamala

Hoja za Nzowa
Kamisha Nzowa anapinga nyumba ambayo anaishi hadi sasa, iliyokuwa na namba 203 na baadaye kubadilishwa kuwa namba 140, kuuzwa kwa Kova kwa kuwa wakati tangazo la kuuzwa nyumba za Serikali linatolewa, yeye ndiye alikuwa akiishi katika nyumba hiyo akiwa mkuu wa upelelezi mkoa (RCO).


Hata hivyo, TBA walimuuzia nyumba hiyo Kova ambaye alikuwa amehamishiwa mkoa wa Kigoma kuchukua nafasi ya RCO.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: