KIVUKO CHA MV KILOMBERO II CHAINGIZWA MAJINI BAADA YA UKARABATI NA MATENGENEZO KUKAMILIKA.
Meneja wa Huduma za Vivuko kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA, Mhandisi Lukombe King'ombe akisimamia zoezi la kuingiza majini baada ya zoezi la ukarabati na matengenezo kukamilika leo majira ya saa 6 mchana na kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd ya Mwanza.
Juma Mtanda, Mwananchi-jmtanda@mwananchi.co.tz
Kivuko cha MV Kilombero II kimeingizwa majini jana majira ya saa 12:53 mchana kisha kufuatia na kazi ndogo za kumalizia kurekebisha ya mifumo ya umeme na usukani kabla ya maandalizi ya mwisho ya kuwasha injini.
Baada ya kumalizika kwa kazi hiyo kitafanyiwa majaribio endapo ya kazi ya matengenezo kumalizika iliyofanywa na kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd ya Mwanza katika kando ya mto Kilombero mkoani Morogoro.
Akizungumza na mwandishi wa Mwanandishi eneo la mto Kilombero wilayani hapa, Meneja Mfuatiliaji wa Vivuko Vilivyoibuliwa kampuni ya Songoro Merine Transport Ltd ya Mwanza, Hemed Koronzo (39) alisema kuwa kazi kubwa iliyokuwa inafanywa ni matengenezo ya kivuko ambayo ilimalizika juzi na jana kazi iliyokuwa mbele yao ni kuingiza kivuko majini.
Koronzo alisema kuwa wafanyakazi wa kampuni hiyo imewachukua wiki mbili kutengeneza na kukarabati kivuko ikiwemo kuziba matundu ya awali na mapya baada ya kupata ajali na kupinduka januari 27 mwaka huu majira ya saa 1 jioni katika mto huo na kusababisha hasara mbalimbali ikiwemo watu kufa maji.
"Kazi kubwa kwetu ilikuwa matengenezo na ukarabati wa kivuko kwa kuziba matundu ya zamani na mapya baada ya kivuko kupata ajali na kazi hizo ni kuziba matundu katika kifua cha kivuko na matenegenezo mengine".alisema Koronzo.
Koronzo alisema kuwa matenegenezo hayo ni pamoja na kujenga milango ya kutokea abiria na magari, kujenga vibanda vya kupumzikia abiria na viti vyake, kupanga rangi, kujenga nguzo za kingo za kivuko na nyingine.
Kwa upande wa Meneja wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Magrath Mapela alisema kuwa hesabu za kuingiza majini zilipangwa kuingizwa mapema wiki lakini kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza imelamizika kuingiza leo (jana) majini.
Mhandisi Mapela alisema kuwa kazi ndogo ndogo za kumalizia kivuko hicho ndizo zilizosababisha kutoka juzi (jumatatu) hadi leo (jumatano) lakini tunashukuru zoezi la kuingiza kivuko majini zimekamilika na limenda salama na kazi iliyobakia kwa mafundi wa Temesa ni kurekebisha mifumo ya umeme na mfumo mzima wa usukani.
"Jioni hii tunatazimia kuwasha injini lakini ni baada ya kumalizika kwa kazi kurekebisha mifumo ya umeme na ile ya mfumo mzima wa usukuni na kufuatiwa na uwashaji wa injini kwa ajili ya majaribio yetu kabla ya SUMATRA kufanya majaribio ya mwisho ili kutoa ruhusa ya kuanza kazi kwa kivuko hiki".alisema Mapela.
Mapela aliongeza kwa kusema kuwa kivuko hicho kilisitisha kazi ya kuvusha abiria na mali zake baada ya kukumbwa na upepo mkali uliombatana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha majira ya saa 1 jioni na kusababisha hasara mbalimbali ikiwemo watu wawili kufa maji na magari matatu kutumbukia mtoni.
magari hayo ni landcruiser mbili ambazo zimeopolewa na fuso moja ambalo bado halijaopolewa mpaka leo lakini baada ya kivuko hicho kutokea eneo la ajali itatoa fursa ya kufanyika kazi ya kuopoa fuso bila vikwazo.
0 comments:
Post a Comment