BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MDUDU KUNGUNI AWASUMBUA WANASAYANSI WAKATI WA JITIHADA ZA KUMUUA.

Wanasayansi wameorodhesha vinasaba vya DNA vya kunguni ili kusaidia kumuangamiza mdudu huyo, ambaye amekuwa akijenga kinga dhidi ya dawa za wadudu.

Matokeo yanaonyesha mdudu huyo anavyoweza kuishi kwa kutengeneza viumbe vinavyokabiliana na sumu ya dawa hizo.

Mdudu huyo pia ameanza kumea ngozi nzito ambayo huwasaidia kujilinda dhidi ya shambulio la kemikali.

Hatahivyo kuna awamu ya maisha yake ambapo ni huenda ikawa rahisi kumuua.
Hii ni kulingana na makundi mawili ya wanasayansi walio na kambi zao kuu katika jengo la makumbusho la Marekani ,Chuo kikuu cha Cincinati pamoja na Taasisi ya Baylor mjini Texas.

Huyo ni kunguni mdogo ambaye hajawahi kuonja tone la damu ya binaadamu.

Kunguni huishi kwa kunywa damu ,na ni hadi mdudu huyo anapoanza kula ndiposa baadhi ya vinasaba vyake vya DNA vinavyomlinda dhidi ya dawa hizo huanza kujiimarisha.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: