Juma Mtanda
news@thecitizen.co.tz
Kilombero.Kikosi cha uzamiaji na uokoaji cha kampuni ya M. Divers Ltd Dar es Salaam kimekabidhi kivuko cha MV Kilombero II baada ya kazi ya kukiopoa majini na kukifikisha nchikavu katika pwani ya mto Kilombero kumalizika rasmi Februari 8 mwaka huu majira ya saa 1:18 jioni mkoani Morogoro.
Akizungumza na gazeti hili eneo la kivukoni Ifakara, Mkuu wa kikosi hicho, Hafidh Seif alisema kuwa kazi kubwa iliyokuwa imebakia ni kumalizia kuyaondoa maji katika matanki manane ya kivuko na kufuatia na zoezi la kukivuta hadi nchikavu na mitambo.
Seif alisema kuwa zoezi la kuondoa maji katika matanki hayo ilichukua muda wa masaa 9:18 zoezi ambalo lililoanza majira ya saa 5 asubuhi na kufikia tamati majira ya saa 1:18 februari 8 mwaka huu.
“MV Kilombero II kimechukua siku 12 mpaka kukinasua, kukiibua na baada ya kazi hiyo tulikiweka katika asili yake na zoezi la kuondoa maji kwenye matanki ilichukua siku tatu tunamshukuru mungu kazi imemalizika salama.”alisema Seif.
Meneja wa Wakala wa Umeme na Ufundi mkoa wa Morogoro (Temesa) Mhandisi, Magreth Mapela akizungumza na Mwananchi alieleza kuwa baada ya kupinduka kivuko hicho injini ya kulia imepata hitilafu.
Mapela alisema kuwa kutokana na injini hiyo kupata matatizo tayari mafundi wa temesa wanafuatilia injini nyingine iliyopo Songea ili kuletwa na kufungwa katika kivuko cha MV Kilombero.
Aliongeza kwa kusema kuwa wanatarajia baada ya wiki mbili zijazo zoezi la matengenezo litakuwa limekamilika na kivuko kitaanza kazi ya kuvusha watu na mali zao.
Mhandisi huyo alisema kuwa mzamiaji wa kampuni ya May-Marine Go Ltd, Yahya Mohamed Omari ameendela na kazi ya kutafuta gari aina ya fuso ambalo lilitumbukia majini.
"Fuso lilishindikana kutolewa mapema kwa sababu eneo lilipotumbukia lilikuwa jirani na kivuko hivyo ni lazima kivuko kitoke ndipo lenyewe lipate nafasi ya kuibuliwa kirahisiwa.
Kwa upande wa mali nyingine ambazo tayari zimeopolewa ni pamoja na magari mawili aina ya landcruizer, moja mali ya benki ya CRDB na Kilombero Valley Teak Company (KVTC).Alisema Mapela.
Mali nyingine zilizopoa ni bunduki aina ya shotgun M 511A HI-Standard mali ya kampuni ya ulinzi ya Alafa iliyokuwa na marehemu Novatu Namali.
Baada ya kivuko cha MV Kilombero II kupata ajali na kupinduka januari 27 mwaka huu tayari watu wawili wameripotiwa kufa maji akiwemo ulinzi wa kampuni ya Alafa Security Gard Ltd Ifakara, Novatus Namali (35) ambaye mwili wake ulipatikana siku ya tatu baada ya ajali hiyo.
Mwingine ni Dastan Rwegasira mkafanyakazi wa benki ya CRDB tawi la Ifakara ambaye mwili wake haujaonekana mpaka leo.
Timu ya wahandisi na mafundi wamewasili katika mji mdogo wa Ifakara ili kufanya kazi ya kukichuguza na kukifanyia matenenzo.
0 comments:
Post a Comment