1, Usitangaze udhaifu wa mkeo kwa familia na marafiki, kila mmoja anamtunzia mwenziwe hadhi yake.
2, Usiwe na mtizamo mbaya wala kuzungumza naye kwa hisia kali huwezi kujua atatafsiri vipi.!
3, Usimlinganishe mkeo na wanawake wengine, huwezi kujua hao wanawake wengine wanapitia hali gani kimaisha.
4, Usisahau kwamba ni mkeo umemuoa, yeye si kijakazi, muhudumie kama malikia na atauonyesha ulimwengu kwamba Mumewe ni mfalme na utamtawala
maishani.
5, Mpe kipaumbele na ni wajibu wako binafsi kumfanyia jambo na sio watu wengine.
6, Usimlaumu mbele za watu hata kama kakosea, mlinde, muhimize, mrekebishe faraghani, ukifanya hivyo kamwe hatokusahau.
7, Usimnyime huduma za kitandani kwa kujifanya mgonjwa/kuchoka ama kutokuwa na hamu. Kumbuka wanaume wengine wanatafuta nafasi hiyo.
8, Usimlinganishe mkeo na mtalaka wako ama mkeo aliyefariki maana wewe ni mume wa pekee kwake.
9, Usimkemee wala kumkosoa mbele ya watoto, ni malezi mabaya kwa watoto maana wewe ni Mwalimu wao, wanakutazama wewe japo unadhani ni watoto tu!.
10, Mtazame mkeo kama kavaa vizuri
kabla hajatoka maana akipendeza
yeye na wewe unaheshimika na
ukipendeza wewe yeye anaheshimika.
11, Usikubali marafiki kuwa karibu na
mkeo, weka mipaka maana hujui nia
zao.
12, Usitoke kuoga na haraka haraka
ukavaa nguo ukatoka pasi yeye
kukukagua, mkeo kazungukwa na
wanaume wanadhifu wanaojali
mazavi na utanashati.
13, Wazazi, ukoo na marafiki sio
waamuzi kwa mambo ya mkeo,
usipoteze muda kutafuta uamuzi wa
mwisho kutoka kwao, ithibiti Ndoa
yako.
14, Mapenzi yako yasiwe kwa sababu
ya mazingira au kihali hata kama
ulimuoa kwa misingi hiyo kwa sasa ni
mkeo mpende bila masharti. Hali
uweza kubadilika na ikiwa ndio msingi
basi ndoa itavunjika.
15, Mkeo anahitaji umakinike kwake
na umsikilize kama mtoto, usiwe mkali
msikilize kwa makini na atakupenda.
16, Usijilinganishe na mkeo, yeye ni
mke kwa hivyo msaidie tu maana
ndoa ni kusaidia.
17, Usimuhukumu mkeo, ni msaidizi
wako na kiumbe dhaifu mchukulie
kwa mtazamo huo na utapata utulivu
wa akili.
18, Mume mzembe hajali. Haogi.
Jiweke nadhifu ukiwa na yeye nukia
vizuri, harufu mbaya inamkirihisha ila
hawezi kukwambia.
19, Usiwe na urafiki na waume walio
na mtazamo mbaya kuhusu Ndoa.
Watakuharibu mawazo.
20, Mkeo ana thamani kubwa sana
ndio maaana ukatoa vitu vya thamani
kumuoa. Penzi lenu lifanye jipya,
uzembe haufai.
21, Kuzaa ni majaaliwa, mpende mkeo
awe na watoto au asiwe nao,
usiwabague watoto kwa jinsia
wafunze dini na watakuwa wacha
Mungu hadi maishani mwao.
22, Hauwi mzee kwa mkeo katika
kumburudisha, usiwe na ugomvi naye
mutakuwa katika kheri. Usiwache
kuwajali watoto wako na mkeo kwa
sababu ya wanawake wengine au
sababu yoyote ile. Wao ni wewe na
wewe ni wao.
23). Mume anayedumu na ibada ana
usalama, omba kila siku, muombee
mkeo na watoto.
TUKIYFANYA HAYA TUTAKUWA NA
NDOA ZA FURAHA KAMA MITUME.

0 comments:
Post a Comment