BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ASKARI POLISI WAWADHIBITI VIJANA WAKOROFI KATIKA MATUKIO YA KUPORA MALI ZA RAIA MAARUFU KAMA 'Panya Road' 18 TANZANIA.

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi linawashikilia vijana zaidi ya 18 wenye umri kati ya miaka 14 na 20 kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya uhalifu katika maeneo ya Wilaya ya Temeke.

Kamanda wa polisi wa Temeke, Gilles Muroto amesema leo kuwa vijana hao, wanaohusishwa na kundi la Panya Road linalofanya unyang'anyi maeneo ya jiji la Dar es Salaam, walikamatwa jana nyakati tofauti baada ya polisi kuendesha msako wa kuzuia na kupambana na wahalifu.

Alisema vijana hao wanatoka maeneo ya Buza Kanisani, Chanika, Yombo Kirakala, Buza Changulu, Yombo Makangawe na moja anayeishi maeneo ya Mwananyamala lakini alikamatwa Temeke.

"Kama Kamanda Simon Sirro alivyosema kuwa ni lazima wahalifu wadhibitiwe katika mkoa huu. Temeke hatuwez kumwangusha, tunatekeleza agizo lake," alisema Kamanda Muroto.

Alisema vijana hao wanajihusisha na vitendo vya uporaji wa mali mbalimbali kuanzia mitaani, pia kujeruhi watu hali inayosababisha wakazi wa eneo husika kuishi kwa hofu.

Alisema upelelezi ukikamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria. 


Wakati huohuo, Kamanda Muroto amesema polisi inashikilia mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 38, mkazi wa Buza baada ya kumkuta na puli 120 za dawa za kulevya aina ya bangi.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: