
Katibu Mkuu Kiongozi, John Kijazi. Picha na Mtandao
Dar es Salaam. Katibu Mkuu Kiongozi John Kijazi amewataka makatibu tawala 10 walioapishwa na Rais John Magufuli leo, kwenda kujifunza changamoto zinazowakabili wananchi kabla ya kuanza mambo mapya.
Walioapishwa leo asubuhi ni Richard Kwisega (Arusha), Selestine Gesimba (Arusha), Armatus Msole (Kagera), Mhandisi Aisha Amour (Kilimanjaro) na Zuberi Samataba (Pwani).
Wengine ni Albert Msovela (Shinyanga), Dk Angelina Lutambi (Singida), Jumanne Sagini (Simiyu), Dk Thea Ntara (Tabora) na Mhandisi Zena Said.
Akizungumza baada ya watendaji hao kuapishwa, Balozi Kijazi amewataka kujifunza changamoto za wananchi na kutatua.
"Mmepata heshima kubwa na jukumu kubwa la kulinda maslahi ya wananchi. Nadhani mnajua hii Serikali ni ya namna gani. Nendeni mkachape kazi," alisema Balozi Kijazi.
Baada ya kuapishwa makatibu tawala hao walikula kiapo cha uadilifu na kuhimizwa kuzingatia masharti yaliyopo katika kiapo hicho.
Naye Kamishna wa Maadili, Jaji Salome Kaganda amewataka viongozi hao kuhakikisha kwamba watumishi walio chini yao wanazingatia maadili ya kazi yao na kujiepusha na mgongano wa maslahi.MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment