BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CHEMBA YA BIASHARA, VIWANDA NA KILIMO YAPASUA JIPU KWA SERIKALI KATIKA KUFIKIA UCHUMI WA KATI KATIKA MILENIA YA MWAKA 2020/2025.

Mwenyekiti wa chemba ya biashara, viwanda na kilimo Tanzania mkoa wa Morogoro (TCCIA) Bachoo Sidik Bachoo akizungumza jambo na waandishi wa habari juu ya Tanzania kuweza kuondokana na uchumi wa chini na kuingia wa kati katika milenia ya mwaka 2020/2025 endapo serikali itapunguza baadhi ya vikwazo kwa wafanyabiashara eneo la Nane Nane Manispaa ya Morogoro, kushoto ni Afisa Mtendaji wa chemba hiyo, Michael Mlambiti.PICHA/JUMA MTANDA

Juma Mtanda, Morogoro.

Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania, tawi la Morogoro limeiionya serikali kuwa viwango vikubwa vya kodi na uwingi wa tozo vitakwamisha juhudi za serikali kufikia malengo yake ya uchumi wa kati ya 2020/2025.

Wameitaka serikali kupunguza vikwazo hivyo ili kuwapa wafanyabiashara nafasi ya kuchangia zaidi katika kukua uchumi.

“Tozo nyingi zinatubana sana sisi wafanyabiashara kiasi kwamba hatuelewi kodi zote hizi tunazotozwa na taasisi zote hizi za nchi zinatusaidia vipi sisi,” alisema Mwenyekiti wa Chemba ya biashara, viwanda na kilimo Tanzania mkoa wa Morogoro (TCCIA), Bachoo Sidik Bachoo.

Akizungumza na waandishi wa gazeti hili mjini hapa, Bachoo ameitaka serikali kupunguza vikwazo zinavyombana mfanyabiashara hasa vinavyotokana na viwango vikubwa na kila aina ya tozo za kodi.

Machoo alisema kuwa baadhi ya taasisi zimekuwa chanzo cha kuzalisha vikwazo vya uanzishwaji wa viwanda vipya na kuwafanya wafanyabiashara kushindwa kuanzisha vyanzo vingi vya mapato.

“Tanzania tunaweza kuondokana na uchumi wa chini na kuingia ule wa kati endapo tu serikali itapunguza lundo la vikwazo vingi vikubwa vya tozo za kodi na kuingia milenia ya mwaka 2020/2025 tukiwa na uchumi wa kati”.alisema Machoo.

Machoo alitaja vikwazo hicho vya tozo kama VAT anayotozwa mfanyabiashara ya 18% ipunguzwe na kufikia 16% ambayo haitamuumiza mfanyabiashara na itasaidia mtumiaji wa bidhaa kuwa na maisha nafuu ambapo kwa sasa maisha yapo juu kutokana na bidhaa kuwa na bei kubwa.

Aliongeza kwa kusema kuwa kodi za bidhaa za nje kodi itozwe 50% ili kuondoa udanganyifu katika ukwepaji wa kodi na serikali itakusanya pesa nyingi kwani hakutakuwa tena na udanganyifu wa wafanyabiashara kukwepa kodi.

Wakati huo huo, Afisa Mtendaji wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania mkoa wa Morogoro (TCCIA), Michael Mlambiti amewatangazia wanachama wenye sifa za kugombea nafasi ya uongozi katika sekta hiyo.

“Uchaguzi tunatarajia kufanyika April 26 mwaka huu na fomu tayari zimeanza kutolewa hivyo tunawaomba wanachama wenye sifa kujitokeza kwa uwingi kugombea nafasi mbalimbali.”alisema Mlambiti.

Mlambiti alisema kuwa uongozi uliopo madarakani tayari muda wao wa uongozi umefikia ukingoni hivyo wanachama wenye sifa wajitokeze kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali.

Alizitaja nafasi hizo kuwa ni pamoja nafasi ya mwenyekiti wa mkoa wakati makamu mwenyekiti nafasi tatu za viwanda, bishara na kilimo, wajumbe sita wa halmashauri ya mkoa na mtunza fedha moja pamoja na wajumbe wawili wa mkutano mkuu wa mwaka.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: