Klabu ya Azam FC imeshindwa kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Africa (CAF) baada ya kufungwa bao 3-o na klabu ya klabu ya Esperance ya Tunisia katika mchezo wa marudiani uliofanyika mjini Rades Tunisia.
Ushindi huo wa wenyeji umeifanya kusonga mbele kwa jumla ya bao 3-2 kufuatia mchezo wa awali uliofanyika Tanzania, Azam FC kushinda kwa bao 2-1 ulipigwa Chamazi Dar es Salaam.
Kabla ya mchezo huo Azam FC walikuwa wakihitaji ushindi au sare yoyote ya magoli ili waweze kusonga mbele.
Esperance walipata mabao kupitia kwa Bguir, Jouini na Errouge kufuatia kutolewa kwa klabu ya Azam FC, Tanzania inabakia na mwakilishi mmoja pekee katika michuano ya kimataifa ambaye ni klabu ya Dar esa Salaam Young Africans inayocheza leo majira ya saa 3:30 usiku majira ya afrika mashariki April 20 katika mchezo wa marudiano na wenyeji wake Al Ahly.
Mchezo wa awali Yanga na wapinzani wao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 huku Yanga ikitakiwa kupata ushindi ama sare ya bao 2-2.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / michezo /
slider
/ HESABU ZA AZAM FC ZAPWAYA MBELE YA ESPERANCE DE TUNIS KOMBE LA SHIRIKISHO BARANI AFRICA KWA KUKUBALI KIPIGO CHA BAO 3-0.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment