Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzanaia Dr.John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa mkoa wa shinyanga Ana kilango Malecela kuanzia leo.
Utenguzi huo umetokana na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Ana kilango Malecela kutungaza kwenye vyombo vya habari kuwa mkoa wake hauna watumishi hewa jambo ambalo lilisababisha Ikulu kufanya uchunguzi wake na kubaini kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya kwanza na awamu ya pili ya uchunguzi bado inaendelea.
Akiongea Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akipokea hundi ya shilingi bilioni sita zilizotolewa na Ofisi ya Bunge baada ya kubana matumizi kwa ajili ya kununulia madawati Rais Magufuli ameeleza kusikitishwa na hali hiyo na kuagiza Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala wa Mkoa kuondolewa ofisini mara moja.
0 comments:
Post a Comment